Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Baada
ya dili la Paris Saint-Germain (PSG) kumchukua kocha wa timu ya taifa
ya Urusi Fabio Capello kuota mbawa, sasa klabu hiyo imekaa meza moja na
kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc ili kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti anayetimkia Real Madrid.
Huo
ni mpango B kwa PSG kwani malengo yao yalikuwa kwa Capello, na sasa
mabingwa hao wameamua kumchukua Blanc mwenye mvua 47 ambaye alikuwa
mlinzi wa zamani wa mabingwa wa soka nchini England, Manchester United.
Mtandao wa kimichezo wa beIN ambao unamilikiwa na wamiliki wa klabu ya PSG wa Qatari Sports Investment company ametoa taarifa hizo mapema leo.
Shavu hilo: Laurent Blanc alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa
Makubaliano
ya kuwa kocha wa PSG yamefikiwa leo kati yake na klabu hiyi na sasa
ataiongoza kutetea taji la ligi 1 walilotwaa msimu uliopita.
Makubaliano hayo ni kuwa kocha huyo ataifundisha PSG kwa miaka miwili na anatarajiwa kusaini mkataba wiki ijayo.
Blanc aliitumikia Manchester United kwa muda wa miaka miwili na kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 2003
0 comments:
Post a Comment