Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mourinho
“byee byee’” Real Madrid!, amemaliza kazi, sasa njia nyeupe kurudi zake
kuelekea darajani nchini England kurithi mikoba ya kocha wa muda wa
chelsea Rafa Benitez.
Ushindi
wa mabao 4-2 dhidi ya Osasuna ambao klabu ya Real Madrid imepata katika
mechi ya kufunga pazia la Ligi kuu nchini Hispania usiku huu, umemfanya
kocha wa klabu hiyo Mreno Jose Mourinho aage kwa furaha baada ya
kuruhusiwa kuondoka klabuni hapo na kutajwa kurejea katika klabu yake ya
zamani ya Chelsea ya nchini Uingereza.
Mabao
ya Real Madrid yametiwa kimiani na wachezaji Gonzalo Higuain dakika ya
35 kipindi cha kwanza, Mickael Esien katika dakika ya 38, Karim Benzema
dakika ya 69 na Jose Maria Callejon.
Kipute
hicho cha mwisho kwa Mourinho akiwa kocha wa Real kimepigwa katika
dimba la Nyumbani Santiago Bernabeu na kushuhudiwa na mashabiki lukuki
wa miamba hiyo ya soka barani ulaya.
Katika
mchezo wa leo nyota kadhaa wa Real Madrid hawajatia madaluga yao
uwanjani akiwemo mchezo nyota Mreno Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo
anayesumbuliwa na majeruhi.
Nyota huyo anawindwa na klabu yake ya zamani ya Manchester United pamoja na wazee wa darajani Chelsea.
Umekuwa
historia nzuri kwa Mourinho ambaye ameandika katika mtandao wa klabu
hiyo akiaga kwa ushindi mnono dhidi ya Osasuna baada ya kukaa miaka
mitatu nchini Hispania akinoa makali ya Real Madrid.
Baada
ya kumalizika kwa mechi, Mourinho ambaye amekubali kurejea Chelsea
msimu ujao wa ligi kuu nchini England aliwapungia mkono mashabiki wa
klabu yake akiwapa mkono wa kwaheri.
Akizungumza
na wanahabari Mourinho amekaririwa akisema “Natamani kuwaona mashabiki
wa Real Madrid wakiwa na furaha wakati wote. Nawashukuru sana mashabiki
wa sapoti yao, naheshimu walivyokuwa wananikosoa. Narudia tena
nawatakiwa mashabiki furaha zaidi na afya njema kwao”.

Kazi imemalizika: Jose Mourinho akiwa kocha wa Real Madrid kwa mara ya mwisho usiku huu katika dimba lake santiago Benabeu

Waandishi wa habari wakimpiga picha za mwisho kocha Jose Mourinho akiwa kocha wa real Madrid kwa mara ya mwisho

SHANGWE
NA MAJUNGU KAMA KAWAIDA!: Mourinho amesalimiwa kwa mgawanyiko uwanjani,
kuna waliomshangilia na walioonesha kutofurahishwa na tabia za kocha
huyo klabuni hapo, duniani huwezi kupendwa na watu wote.
WAMEMKUBALI
SANA JEMBE : Mashabiki wa Real Madrid wakipeperusha bendera ya
Mourinho kuonesha heshima kwake na kukubali kazi yake klabuni hapo.


JEMBE
LINASEPA: Mashabiki wa Real Madrid wakishika makaratasi yenye ujumbe wa
shukurani kwa kocha Jose Mourinho anayeondoka klabuni hapo

KILA LA HERI: Mourinho akiwaaga mashabiki wa Real Madrid baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa



Jembe halijacheza leo: Ronaldo aliachwa katika kikosi cha leo kutokana na majeruhi

MASHINE YA SANTIAGO: Ronaldo aliingia uwanjani na kuwasalimia mashabiki wa klabu yake

Bao la kuongoza: Gonzalo Higuain akipongezwa baada ya kutia gozi kimiani

0 comments:
Post a Comment