Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha mkuu wa klabu ya Napoli ya Italia
Rafael Benitez amemtaka mshambuliaji wake nyota Edinson Cavani
kuendelea kuichezea klabu hiyo kwani bado anapendwa sana, ingawa amekiri
kuwa kumuuza hakukwepeki kama ofa nzuri itatolewa na klabu
inayomhitaji.
Kocha
huyo wa zamani wa Inter Milan na Chelsea amerudi katika ligi ya Italia,
Seria A ili kuisaidia Napoli kuwania ubingwa wa ligi ambapo kocha
aliyetimka klabuni hapo Walter Mazzarri alipata nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Juve msimu uliopita.
Cavani,
mwenye umri wa miaka 26, aliifungia klabu yake mabao 29 katika michuano
ya ligi kuu ya Italia na sasa klabu za Manchester City, Chelsea na Real
Madrid zinapigana vikumbo kuhakikisha zinainasa saini ya nyota huyo.
Baki, baki, baki: Rafa Benitez (chini amemtaka Edinson Cavani kubakia Napoli na kukataa ofa ya Chelsea
Benitez ameliambia gazeti la Corriere dello Sport: ‘Tunamtaka Cavani kukaa Napoli”.
“Cavani anajua jinsi gani anapendwa na kuwa na thamani kubwa ndani ya klabu hiyo” Alisema Benitez.
Pia Benitez
amemshukuru sana mshambuliaji wake wa zamani katika klabu ya Liverpool
na Chelsea Fernando Torres kwa kushirikiana naye sana wakati akiwa kocha
wa muda wa Chelsea msimu uliopita.
Cavani amekuwa mchezaji muhimu sana katika klabu ya Napoli
0 comments:
Post a Comment