Mabingwa
wa Ligi Kuu ya England wamekubaliana na mchezaji huyo kumlipa mshahara
wa Pauni Milioni 5.5 kwa mwaka kupitia kwa baba yake Thiago, aliyewahi
kutwaa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Brazil, Mazinho, na wana
uhakika wa kumalizia dili kwa kuilipa Pauni Milioni 17 klabu yake ya
uhamisho.
Barca
bado ina matumaini ya kumbakiza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa
kumuahidi atakuwa kiongozi klabu hiyo kwa miaka ijayo, lakini anabakia
kuwa asiyeshawishika baada ya kusotea namba kwenye kikosi cha kwanza.
Anabaki, habaki: Thiago Alcantara, akiwa na taji la Ulaya la U21, tayari amekubaliana na Manchester United
Thiago
amekwenda mapumzikoni, akimuacha baba yake na wawakilishi wake
wazungumze na mabingwa hao wa Hispania, ambao wanatarajiwa kuiambia
Barcelona kwamba wanataka kutoka Nou Camp kuhamia Old Trafford.
United imefanya jitihada kubwa kuhakikisha inampata mchezaji huyo, ikiamini Manchester City na Bayern Munich wanaweza kutoa ofa.
Inafahamika
hawana mpango na mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani lakini
wanaendelea kufuatilia sakata la Mkataba wa Cristiano Ronaldo Real
Madrid.
Nyota
huyo wa zamani wa United, ameahidiwa Pauni Milioni 12 kwa mwaka ili
abaki Bernabeu, lakini anataka Milioni 5 zaidi na hajafirahishwa na
maneno ya karibuni ya Rais wa Real, Florentino Perez kwamba kila kitu
kina kiwango chake.
Shujaa anarudi? United inaangalia uwezekano wa kumrejesha Cristiano Ronaldo
Kocha mpya: David Moyes anataka kujenga kikosi imara kabla ya kuanza kazi rasmi United
0 comments:
Post a Comment