Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli alifunga bao la ushindi kwa Italia, baada ya Andrea
Pirlo kutangulia kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa adhabu akiichezea
nchi yake mechi ya 100 katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mabara.
Balotelli
alipokea nzuri ya Emanuele Giaccherini zikiwa zimesalia dakika 12 na
akapasua katikati ya mabeki wawili kabla ya kufunga kwenye Uwanja wa
Maracana.
Mshambuliaji
wa Manchester United, Javier ‘Chicharito’ Hernandez alifunga kwa
penalti dakika ya 34 kuipa Mexico bao la kusawazisha baada ya Andrea
Barzagli kumuangusha kiungo wa zamani wa Tottenham, Giovani Dos Santos
kwenye boksi.
Hernandez anaelekea kuipiku rekodi ya mabao mengi Mexico, 42 yaliyofungwa na gwiji wa zamani wa nchi hiyo, Jared Borgetti.
Mchezaji
bora wa mechi alikuwa Pirlo aliyefunga bao la kwanza dakika ya 27
akimtungua kwa mpira wa adhabu kipa wa Mexico, Jose de Jesus Corona.
Kikosi
cha Mexico kilikuwa: Corona, Rodriguez, Salcido, Flores, Moreno,
Torrado, Aquino/Mier dk53, Zavala/Jimenez dk85, Guardado, Giovani na
Hernandez.
Italia: Buffon,
Chiellini, De Sciglio, Abate, Barzagli, Marchisio/Cerci 68, De Rossi,
Montolivo, Pirlo, Giaccherini/Aquilani dk88 na Balotelli/Gilardino dk85.


Balotelli akiandika bao kimiani


Mpenzi wa Balotelli, Fanny Neguesha akifurahia mechi kwa kupiga picha

Javier ‘Chicharito’ Hernandez aliifungia kwa penalti Mexico
0 comments:
Post a Comment