Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Lejendari
wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Real Madrid ambaye kwa sasa ni
mkurugenzi wa michezo wa miamba hiyo ya Hispania, Zinedine Zidane
amemuomba mshambuliaji nyota wa klabu ya kaskazini mwa London, Tottenham
Hospur, Gareth Bale kuiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka ili
kuongeza kasi ya dili la kusajiliwa Santiago Bernabeu.
Zidane
amepewa kazi ya kuhakikisha wanamnasa mchezaji huyo hatari ambaye ni
chaguo namba moja kwa miamba hiyo ya soka la Hispania.
Taarifa
kutoka Spurs zinaeleza kuwa Bale mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa, bado
ana furaha ya kuwepo White Hart Lane licha ya timu yake kushindwa
kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya mwakani.
Lakini
Zidane anaamini kuwa Bale kujiunga na miamba hiyo yenye mafanikio
barani ulaya itakuwa vizuri kwake, hivyo ailazimishe klabu yake kumuuza
katika majira ya joto ya usajili.
“Nadhani
Real Madrid imevutiwa na Bale, hilo halina ubishi kabisa, na klabu
haina shaka na ada ya usajili, ipo tayari kumwaga kitita kikubwa ili
kumnasa nyota huyo”. Zidane ameliambia gazeti la Sunday.
Zidane
ameongeza kuwa kama Bale anafikiria kuwa ni muda wake kuhama, basi
aongee na viongozi wa klabu yake ili taratibu zikamilike.

Real Madrid wamekufa wameoza kwa nyota huyu ambaye msimu uliopita alitwaa tuzo mbili za uchezaji bora nchini England

Mali ya moto: Bale ni chagua la kwanza la usajili wa Real Madrid
Mapema
wiki hii, mchezaji wa zamani wa Tottenham Luka Modric alikaririwa na
vyombo vya habari kuwa Bale ataendana na mfumo wa Real Madrid, hivyo
akubali kujiunga nao.

0 comments:
Post a Comment