Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA Andre Villas-Boas ameripotiwa kupiga chini ofa ya kuifundisha Paris Saint-Germain ili abaki Tottenham.
Mabingwa
hao wa Ufaransa walitaka Mreno huyo arithi mikoba ya Carlo Ancelotti,
anayeelekea Real Madrid, lakini sasa wamehamishia mawindo yao kwa Fabio
Capello.
Inafahamika
Villas-Boas alipewa ofa ya Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa
Qatari wanaoimiliki PSG baada ya majadiliano na wakala wake, Carlos
Goncalves, lakini mwalimu huyo kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo
adimu Spurs waliomchukua msimu uliopita baada ya kutupiwa virago
Chelsea.
Tottenham
wanatarajiwa kubomoa benki kumpa fedha za kutosha Villas-Boas,
aliyebakiza miaka miwili katika Mkataba wake White Hart Lane, ili
kujenga kikosi cha nguvu cha kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Miongoni
mwa wachezaji anaowataka ni kiungo wa Corinthians, Paulinho, wakati
Spurs pia ni klabu pekee iliyoomba kumsajili kiungo wa Atletico Mineiro,
Bernard. Wakala wake amesema: “Dortmund hawajawasilisha mapendekezo na
Tottenham ni washindani pekee,”.
Villas-Boas
pia inaelezwa anavutiwa na ushindani wa kupambana na bosi wake wa
zamani, Mreno mwenzake Jose Mourinho katika Ligi Kuu England msimu ujao
Anabaki: Villas-Boas ameripotiwa kubaki White Hart Lane
Kazi ya kufanya: Villas-Boas anataka kuipaisha matawi ya juu zaidi Spurs kutoka nafasi ya tano aliyowapa msimu uliopita
Mpango B: Kocha wa Urusi, Capello anaweza kuwa kazini msimu ujao
Taarifa
za jana usiku nchini Ufaransa zinasema kocha wa zamani wa England,
Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG kwa Mkataba wa mwaka mmoja
Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
Urusi
ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia
mwakani nchini Brazil,na kuna uwezekano Capello akarejea katika timu
hiyo ya taifa baada ya msimu mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake
katika Kombe la Dunia.
Carlo Ancelotti anatarajia kuhamia Real Madrid
Msimu mzuri: PSG walikuwa mabingwa Ufaransa na wanataka kujiimarisha zaidi
0 comments:
Post a Comment