Bi
Rehema Shauri Madongo mkazi wa Wilolesi mjini Iringa akiwa na mtoto
wake baada ya kuponea katika tundu la sindano kuuwawa kwa kipigo
kutoka kwa mmewe ambaye ni askari polisi mjini Iringa kiasi cha
kukimbia nyumba na kurudi kwa wazazi wake
stepen kanyala akiwa na mke wake siku ya harusi yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa
Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri |
IGP Mwema
WAKATI
jeshi la polisi nchini likiendelea kujiweka karibu na Raia hata
kuamua kuanzisha dawati la jinsia katika vituo vya polisi ,kwa
mkoa wa Iringa baadhi ya askari wanadaiwa kupiganga na jitihada hizo
za polisi kwa kushindwa kuheshimu dawati hilo na badala yake
kushiriki kulivunjia heshima jeshi hilo kutokana na kufanya vitendo
ambavyo ni kinyume na mkakati wa jeshi hilo katika kuanzisha dawati la
jinsia.
Uchunguzi
wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com na
www.francisgodwin.blogspot.com umeonyesha kuwa dawati hilo kwa
askari limekosa kuheshimika kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa
kijinsia ambavyo baadhi ya askari (30) wamekuwa wakifanya kwa watoto
wao na wake zao.
Rehema
Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa
na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi
alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa
kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote
zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .
”
Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo
cha upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo
nilianza kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso
makali niliyokuwa nikiyapata”
Anasema
kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume
wake huyo hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake
ambazo zimetoka kwa wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa
kwa kipigo kikali.
Rehema
alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa
kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .
Kwa
alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya
zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu
zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo
amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba .
”
Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa
nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo
kikali kimekuwa kikinikuta ….hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20
na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara
moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa
wazazi nimerudi mara tatu sasa”
Alisema
kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo
amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi
kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda
ukatili wa kinyama.
Hata
hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo
ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga
kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua .
Alisema
kuwa baada ya kujifungua mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume huyo
alimpiga kiasi cha kumjeruhi mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi
ambalo lilielekezwa kwake na bahati mbaya likaishia kwa mtoto.
Aidha
alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji
unaofanyika kutokana na polisi kulindana na kuwa suala hilo la
askari polisi kulindani lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa
Evarist Mangala ,pia alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa
sasa amehamishwa baada ya cheo kupanda pia amepata kufikisha
malalamiko yake ila hakuna jipya ila sasa amefikisha tena suala
hilo kwa kamanda mpya RPC Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika kulishughulikia suala lake
Pia
alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua
kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari
huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake .
Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .
Kwa
upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa
amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati
mwanaume huyo amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.
Hivyo
alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa
wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja
kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo
amekuwa akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku
wataonja mauti.
Bi
Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na
Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa
sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo .
Hivyo
aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama
kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa
Iringa ila askari wenzake wanamlinda.
Kuhusu
uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na
binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari
kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili
kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto wake huyo.
………………Itaendelea ……….
0 comments:
Post a Comment