
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na naibu katibu mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Zitto Kabwe ameoneshwa kushangazwa na serikali
kugawa vitalu vya mafuta na gesi asilia kabla ya wabunge kushirikishwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,Mheshimiwa Zitto
amesema hatua iliyochukuliwa na serikali inapingana na maamuzi ya bunge ambayo
ilizuia ugawaji wa gesi asilia mpaka sera na sheria ya nishati hiyo
ikamilishwe.
Mbunge huyo amesema zabuni hiyo ya utafutaji wa mafuta na gesi
asilia ni vile vilivyoko kwenye Bahari
kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.
Mheshimiwa Zitto amesema wabunge wamealikwa kwenye semina ya
gesi asilia lakini litakuwa ni jambo la kushangaza kama wabunge watakimbilia
posho za semina hiyo na kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa
Kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha amewashauri wabunge kupinga kwa nguvu zote uamuzi wa
serikali wa kugawa vitalu vipya bila
kwanza kuwepo Kwa sera na Sheria mpya ya mafuta na gesi asilia.
Wakati semina ikifanyika jumamosi wiki hii tayari wizara ya nishati na madini ikitaraji kuwasilisha baje
22 - 23 Mei 2013.
0 comments:
Post a Comment