Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuipongeza Yanga kutwaa ubingwa msimu wa 2012/2013. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa TBL Ilala michikichini jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni katibu mkuu wa Yanga Lawreence Mwalusako (katikati) na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga,
Na Baraka Mpenja
Mabingwa
wa ligi kuu soka Tanzania bara na mabingwa watetezi wa kombe la Kagame,
klabu ya Yanga ya Dar es salaam wamepewa zawadi ya sh. Milioni 25
kutoka kwa wadhamini wakuu wa klabu hiyo, Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), wameizawadia klabu hiyo Sh. Milioni 25 kwa kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara uliomalizika mei 18 mwaka huu.
TBL,
wanaoidhamini Yanga na Simba kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager
imekabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milion 25 leo kwa Yanga katika hafla
iliyofanyika ukumbi wa Safari Pub, uliopo makao makuu ya TBL, Ilala, Dar
es Salaam.
Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe wakati akikabidhi
mfano wa hundi hiyo alisema Kilimanjaro Premium Lager imefurahishwa sana
na ubingwa wa Yanga na kusema imejizatiti kikamilifu kuisaidia timu
ambayo imeibuka bingwa katika ligi yenye ushindani mkubwa kutokana na
kuibuka kwa timu mpya zenye nguvu.
“Yanga
imekuwa akionesha soka safi kwa kipindi chote, ligi ni ngumu sana
lakini wamecheza soka maridadi, hivyo kuibuka mabingwa sio ajabau
kabisa. Napenda kuwapongeza wachezaji wa Yanga, kocha na Uongozi mzima
wa Yanga kwa matokeo mazuri ya kushinda Ligi kuu kwa mara ya 24 sasa.”
Alisema Kavishe.
Kavishe
aliongeza kuwa zawadi hiyo ni sehemu ya sh bilioni 1.5 ya udhamini wa
Kilimanjaro Premium Lager kwa Yanga na imetolewa kwa lengo la
kuhamasisha klabu kujitahidi kwa ushindi zaidi na kusaidia klabu katika
maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ambayo tayari Yanga
ina sifa za kushiriki kutokana na ubingwa waliojipatia.
Akipokea
hundi hiyo, Katibu mkuu wa Yanga , Bwana Lawrence Mwalusako alisema
Yanga inaishukuru sana Kilimanjaro Premium Lager kwa mchango wao.
Aliongeza kuwa Yanga ni timu nzuri na yenye nguvu kutokana na uongozi
imara pamoja na udhamini mkubwa kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
‘‘Mafanikio
yetu ya uwanjani ni kielelezo cha mafanikio ya kampuni na pia (TBL) na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa ujumla ambayo imekuwa ikitusaidia
sana.’’ alisema Mwalusako.
Mwalusako
aliongeza kuwa kwa sasa Yanga ina nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la
kimataifa la soka kutokana na mafanikio hayo na kuahidi kujipanga zaidi
kufanbya makubwa zaidi.
Yanga itawakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Kagame.
0 comments:
Post a Comment