Na Baraka Mpenja
Ligi kuu soka Tanzania bara imeendelea leo katika miji ya Dar es salaam, Pwani na mji kasoro bahari Morogoro Tanzania.
Jijini
Dar es salaam zimepigwa mechi mbili ambapo mabingwa wa ligi hiyo klabu
ya Yanga imewakaribisha Wagosi wa Kaya Coastal unioni ya jijini Tanga na
kushuhudia dakika tisini za mchezo huo zikimalizika kwa sare ya
kufungana bao 1-1.
Sasa
Yanga wanasubiri mechi ya mwisho dhidi ya watani zao wa jadi, wekundu wa
Msimbazi Simba “Taifa kubwa” itakayopigwa mei 18 uwanja wa taifa Dar es
salaam.
Huko
Chamazi maafande wa JKT Ruvu waliwakaribisha maafande wa Tanzania
Prisons ya jijini Mbeya na mtanange huo umemalizika kwa Prisons kuibuka
kidedea baada ya kushusha kipigo cha mabao 2-1 na kupanda mpaka nafasi
ya 8 na pointi 29, sasa hawashuki daraja tena.
Mkoani
Morogoro katika dimba la Jamhuri, vibonde wengine wa ligi hiyo Polisi
Morogoro chini ya kocha Rishard Adolf wamewakaribisha Kagera Sugar na
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vijana wa Abdallah Kibaden “King
Mputa” na kusubiri hatima ya JKT Ruvu ambao leo pia wamepigwa chamazi.
Huko
Mashamba ya miwa Manungu Turiani mji kasoro bahari, wakata miwa wa
Mtibwa sugar walishuka dimbani dhidi ya vibonde wa ligi hiyo Africa Lyon
ambapo Mtibwa wameibuka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 huku mabao
yote yakitiwa kimiani na nyota wao aliyerejea baada ya kuwa majeruhi,
Hussein Javu.
Na
huko Mabatini Mlandizi mkaoni Pwani, wanajeshi wa Ruvu Shooting
walipambana na wanajeshi wenzao wa JKT Oljoro na mechi hiyo kumalizika
kwa suluhu pacha ya bila kufungana.
0 comments:
Post a Comment