Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe akiongea na
mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania leo jijini Dar es
salaam alipokutana nao kujadili maandalizi ya mkutano wa Kimataifa wa
Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) na mchango wao
katika kuhamasisha ushiriki wa nchi wanazotoka katika mkutano huo
utakaofanyika mwezi ujao. Kushoto kwake ni Balozi wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo Juma – Alfani Mpango.
Meneja
Mradi wa mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart
Pertinership) Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao leo jijini Dar es salaam kuhusu maendeleo na
maandalizi ya mkutano huo utakaohudhuriwa na wachumi, wanasayansi na
viongozi mbalimbali wa serikali kutoka ndani na nje ya nchi.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
Sehemu
ya mabalozi wakifuatilia hatua mbalimbali za maandalizi ya mkutano wa
Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) na
mchango wao katika kuhamasisha ushiriki wa nchi wanazotoka katika
mkutano huo. Zaidi ya washiriki 500 wanatarajiwa kwenye mkutano huo
utakaojadili kwa kina matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuleta
Maendeleo kwa nchi zinazoendelea.
Meneja
Mradi wa maandalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa
ya Wote (Smart Pertinership) Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa
mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao kuhusu maendeleo na maandalizi ya
mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika mwezi June jijini Dar es salaam
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais 10 kutoka nchi
zilizoendelea.
Sehemu
ya mabalozi wakifuatilia hatua mbalimbali za maandalizi ya mkutano wa
Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) na
mchango wao katika kuhamasisha ushiriki wa nchi wanazotoka katika
mkutano huo. Zaidi ya washiriki 500 wanatarajiwa kwenye mkutano huo
utakaojadili kwa kina matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuleta
Maendeleo kwa nchi zinazoendelea.
0 comments:
Post a Comment