Na Magreth Kinabo – Maelezo
WAZIRI
Mkuu Mizengo Pinda amelipongeza Jeshi la Polisi nchini katokana na
juhudi mbalimbali linalozionesha na kuwataka wabunge kulitia moyo.
Kauli
hiyo ilitolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu Pinda mara baada ya kuwasili
mjini Dodoma akiwa ametokea jijini Arusha baada ya kuwatembelea
majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru,
jijini Arusha ili kuwajulia hali.
Majeruhi
hao walilazwa katika hospitali hiyo kufuatia mlipuko wa bomu ulitokea
lipuko wa uliotokea katika kanisa la katoliki la Mtakatifu Joseph
Parokia ya Olasiti Arusha Mei 5, mwaka huu saa 4:30 na kusababisha
vifo vya watu watatu na majeruhi 69.
”
Jana lilikuwa ninasiliza mjadala wa Bunge nimesikia jeshi la polisi
likiwa linalaumiwa. Chombo hiki kinajitahidi … tuwatie moyo tuwatie
nguvu .Serikali itaendelea kuwasaidia,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Kauli
hiyo pia iliungwa mkono na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera,Uratibu wa Bunge William Lukuvi wakati akichangia mjadala wa
Makadrio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa
mwaka wa fedha 2013/2014.
Wabunge
wengine waliopongeza jeshi hilo , wakati wa mjadala huo ni Richard
Ndassa Mbunge wa Jimbo la Sumwe- CCM, ambaye alisema kama kusingewepo
na juhudi za polisi na uwepo wao wanaotuhumiwa katika tukio la Arusha
wasingekamatwa.
Huku
akimshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne
Makinda kuwa katika maeneo ya nyuma ya jengo la Bunge kwenye maegesho
yaimarishwe ulinzi.
“Nawatia moyo polisi … wanafanya kazi ngumu tunapowabeza hatuwatendei haki,” alisema.
Naye
Aggrey Mwanri, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mbunge wa Jimbo la Siha,
alisema jeshi hilo linafanya kazi vizuri hivyo kinachotakiwa ni
ushirikiano kutoka kwa wananchi.
Kwa
mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Kapteni George
Mkuchika alichangia mjadala huo alisema jeshi askari polisi mmoja
huduhimia raia 1:1100 , twakimu za mitaifa zinaoyesha askari polisi
1:400-600.
0 comments:
Post a Comment