Saturday, May 25, 2013


1
Mzee Ibrahim Akilimali akiongea na waandishi wa habari

Na Baraka Mpenja
Siku chache baada ya mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Klabu ya Yanga ya Dar es salaam kulamba madume mawili katika usajili, Mrisho Khalfan Ngassa “Anko”  na Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima “Fabrigas”  baraza la wazee wa klabu hiyo wameendelea kutia baraka kwa uongozi kwa Yusuf Manji.
Katibu wa baraza la wazee wa klabu hiyo, Mzee Ibrahim Akilimali amesema usajili mzuri unaofanywa na viongozi wao unaleta matumani ya kufanya vizuri ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
“Tunapopanga kikosi chetu tunataka huyu mtoto Ngassa, Twite, na Niyonzima wakae pamoja kufanya maajabu ya soka, timu yetu inajiandaa na michuano ya Afrika mwakani na ndio maana tunafanya usajili makini sana”. Alisema Akilimali.
Akilimali alitamba kuwa jeuri ya pesa waliyonayo Yanga ndio sababu ya kusajili vijana wazuri, na kama mtu anabisha aangalie orodha ya viongozi wa Yanga kama kuna mtu mwenye njaa.
“Mimi nasema viongozi wetu wana uwezo wa kutumia pesa zao kabla hawajatafuta msaada kwa watu wengine, na matokeo yake tutazidi kuwapiga bao wapinzani wetu”. Alitamba Akilimali.
Mzee huyo aliyeongea kwa kujiamini alisisitiza kuwa wakati wanaendesha harakati za kupindua uongozi wa mwana sheria Llod Nchunga, wazee walitangaza kuwa wana fedha kiasi cha milioni mia saba kuiendesha klabu na hivyo mwenyekiti huyo ang`atuke, lakini hawakuwa na maana ya kwamba wao ndio wenye fedha hizo.
“Nilitangaza tunazo milioni mia saba, watu hawakuelewa, maana yangu ilikuwa ni kupata viongozi wenye pesa zao kama Yusuf Manji, Clement Sanga, Binkleb na wengineo ambao ukipima na mzani, thamani yao ni zaidi ya shilingi milioni mia saba”. Alisema Akilimali.
Akilimali aliwataka mashabiki na wanachama wa Yanga kuendelea kuunga mkono jitihada za viongozi wao wakiongozwa.
“Sisi tunabariki sana kazi za mwenyekiti wetu, uongozi wake umetupa matumaini makubwa sana, tutafika mbali zaidi kwa mpango huu”. Alisema Akilimali.
Jana Yanga imetangaza kumsajili Haruna Niyonzima kwa mkataba wa miaka miwili na mei 19 mwaka huu walimtambulisha Mrisho Ngassa masaa machache baada ya pambano la watani wa jadi ambapo Yanga alishinda mabao 2-0.
Simba wanadai Ngassa ana mkataba nao wa mwaka mmoja na Yanga walitangaza kumsainisha mkataba wa miaka miwili na Ngassa alikaririwa akisema ameamua kujiunga na klabu yake hiyo ya zamani yenye makazi yake mitaa ya Twigar na Jangwani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video