Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji
nyota wa klabu ya Manchester United, “Mashetani wekundu” na mabingwa wa
ligi kuu soka England, Wayne Rooney amepata mtoto wa pili usiku wa
kuamkia leo.
Mke wake mpendawa Coleen amejifungua mtoto wa kiume na wamempatia jina la Klay.
Coleen
alipatwa na uchungu jumamosi usiku wiki iliyopita na kumsababisha
Rooney ashindwe kusafiri na timu yake kuifuata West Bromwich katika
kipute cha kufunga pazia la ligi kuu England ambapo mechi hiyo ilimazika
kwa sare ya kufungana mabao 5-5 na kumuaga rasmi kocha wa klabu hiyo
Kibabu Sir Alex Ferguson.
Rooney
alitangaza taarifa hiyo katika mtandao wake wa Twita akiwaambia wafuasi
wake zaidi ya milioni 6 kuwa amefurahi kupata mtoto mzuri wa kiume
Klay Anthony Rooney, huku mama yake na mtoto Klay wakiwa wazima.
Mtoto
wa kwanza wa Rooney ana miaka mitatu mpaka sasa na anaitwa Kai, hivyo
sasa amekuwa baba wa watoto wawili. Hongera sana Rooney.
Wakati
huo kuna taarifa kuwa kocha mpya wa United, David Moyes anatarajia
kukutana muda wowote na Rooney ili kuzungumzia hatima yake klabuni hapo
msimu ujao.
Hivi
karibuni Rooney na Ferguson hawakuwa katika maelewano mazuri mpaka nyota
huyo aliomba kuihama klabu yake hiyo ambayo imempa jina kubwa zaidi
duniani.
SISI NI FAMILIA: Wayne na Coleen Rooney, tayari wameshatangaza ujio wa kidume chao Klay usiku wa kuamkia leo
HONGERA
SANA: Rooney ameandika taarifa hiyo hapo juu katika mtanado wake wa
Twita huku maelefu ya watu wakimpongeza na kumtakia kila la heri
JUU
YAKO DAVID: Kocha mpya wa United Moyes lazima azungumze na
mshambuliaji huyo baada ya kumueleza bosi wake Sir Ferguson kuwa anaomba
kuihama United.
0 comments:
Post a Comment