Na Frank Shija – MAELEZO
Wananchi
wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujitokeza katika maadhimisho ya siku
ya wauguzi dunia itakayofanyika kimkoa katika viwanjwa vya chuo kikuu
cha Dar es Salaam, kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 11 na kufikia kilele
tarehe 12 mei 2013.
Wito
huo umetolewa na mwakilishi wa chama cha wauguzi tawi la mkoa wa Dar
es Salaam Bi. Joan Bigirwa alipokuwa akiongea na waandishi wahabari leo
(jana) jijini Dar es Salaam.
Joan
alisema kuwa kutokana na kaulimbiu ya mwaka huu kuhusu malengo ya
millennia yanahusu vijana wameamua kufanyia maadhimisho hayo katika
viwanjwa vya chuo kikuu ili kutoa fursa kwa vijana wengi kushiriki
katika maadhimisho hayo.
Aidha
amesema kwamba maadhimisho hayo yanataraji kuanza saa tatu asubuhu kwa
maandamano kututoka Ubungo hadi viwanja vya Chuo Kikuu cha na
kupokelewa na mgeni rasmi ambaye atakuwa ni Mstahiki Meya wa jiji la Dar
es Salaam.
Naye
Mwenyekiti wa TANNA tawi la vyuo vikuu Bi. Wilhelmina R. Niwabigira
ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na utoaji wa huduma
mbalimbali.
Niwabigira
ametaja baadhi ya huduma hizo zitakazotolewa ni ushauri nasaha,kupima
saratani ya shingo ya kizazi na matiti,kupima kisukari,afya ya akili,
presha na ushauri wa vicoba ambapo huduma zote zitatolewa bure.
Siku ya wauguzi dunia usherehekewa kila mwaka kwa kumkumbaka mwanzilishi wa uuguzi nchini Bi. Florence Nightngale.
0 comments:
Post a Comment