Daniel
na Mwalimu – Timu pekee kutoka Tanzania iliyobaki katika mashindano ya
Guinness Football Challenge, Mwalimu Akida(kulia) na Daniel
Msekwa(kushoto) tayari kwa nusu fainali ya kesho
Mei
15, 2013 Dar es Salaam, Jumatano iliyopita kupitia televisheni za ITV
na Clouds TV timu ya Ghana iliyoshinda katika kipindi cha Tisa cha
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE walifurahia kupata nafasi katika nusu
fainali kwa kucheza azonto ambayo iliwafanya watangazaji Larry na Mimi
kujiunga nao. Kofi Okarku na Isaac Aryee ingawa hawakufanya vizuri
katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness walifanikiwa
kupata dola za kimarekani 1,500 na waliufanya uwanja wote kunyanyuka na
kucheza.
Timu
iliyoshinda ilifanya vizuri katika hatua za mwanzo na kujipatia alama
16 pamoja na kuonesha uwezo mzuri ufahamu wa soka. Waliwashinda Wakenya
katika hatua ya penati, hata hivyo timu ya Kenya imefuzu nusu fainali
kama washindi wa pili.
Emanuel,
Kenneth, Chris na Isaac wataendelea kuziwakilisha nchi zao katika hatua
ya nusu fainali, wakiwa na ndoto za kufanya vizuri na kuwa washindi wa
Pan-African Guinness Football Challenge.
Meneja
wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi alisema, “Nusu fainali ya kwanza
inatarajia kufanyika wiki ijayo tukisubiri kuona ni nani atakayefanikiwa
kutinga fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Timu kutoka
Dar-es-Salaam,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad watapeperusha bendera
ya taifa letu na kuwakilisha Afrika mashariki hivyo tunawatakia kila
la heri. Tunazisifu timu zote na sasa timu bora zitakutana kuwania
kufuzu kuingia fainali”
Timu zitakazoendelea na michuano ni pamoja na;
KWA WATANZANIA
- NDANI YA JEZI ZA KIJANI-Kutoka Dar-es-Salaam, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao awali walijishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya kitaifa na waliishia katika hatua ya penati kwenye robo fainali wataweza kufikia hatua ya pesa ukutani katika nusu fainali?
KWA WAKENYA
- NYEUSI-Kenneth Kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi.Ken ni kocha na Wills ni dereva.Timu hii ilijishinda katika robo fainali ya pili na kuongeza dola 1,500 kwenye dola 3,000 walizokuwa nazo awali.
- JEZI NYEKUNDU-ni timu ya pili kutoka Kenya,Francis Ngigi kutoka Nairobi na Kepha Kimani kutoka Thika.Timu hii ilipata dola 3,000 katika hatua za kitaifa na walifika hatua ya penati katika robo fainali.
KWA WAGHANA
- JEZI ZA BLU- Timu ya Ghana iliyopata fedha nyingi zaidi katika hatua ya kitaifa, Jonathan Naab kutoka Tindogo na Desmond Odaano kutoka Larteh wamefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kupata jumla ya dola 8,500. Je, watafanikiwa kuingia fainali?
Nusu fainali ya kwanzaitarushwa na televisheni za ITV na Clouds TV usikose kuangalia mchezo huu na kushangilia timu yetu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge nchini wanaweza
kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya
hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia
simu ya mkononi.
Usikose kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na
kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia
kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV
kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment