
Nyota wa Simba wakipasha misuli kujiandaa na kipute cha kesho cha watani wa jadi katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Kocha Mfaransa Patrick Liewig ataoneshana kazi na Mholanzi Ernie


Maarifa ya Mholanzi Ernie Brandts mbele ya maarifa ya Mfaransa wa Simba Patrick Liewig

Patrick Liewig kuiongoza Simba kesho uwanja wa taifa kuwatafuna Yanga
Na Baraka Mpenja
Ilikuwa
inahesabika miezi, wiki, siku na sasa imebaki siku moja tu kushuhudia
watani wa jadi, yaani wekundu wa Msimbazi Simba “Taifa Kubwa”
wakigagaduana vikali na mabingwa Dar Young Africans katika uwanja wa
kisasa wenye sifa zote wa taifa jijini Dar es salaam “Jiji la maji
chumvi” kesho majira ya saa 10 kamili jioni.
Kiputo hicho kinatarajiwa kuwa na burudani kubwa kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wa miamba hii ya soka la Tanzania.
Simba
chini ya kocha Mfaransa Patrick Liewig akisaidiwa na kocha mzalendo
aliyebarikiwa kuwa na maneno mengi Jamhuri Kiwhelu “Julio Alberto”
wanatumia vijana zaidi kuliko wachezaji wakongwe “Mafaza” na hii
imesababisha klabu hiyo kuwa na kikosi chenye makali zaidi hususani
mechi za lala salama, lala kwa buriani za ligi kuu.
Yanga
wao wamechangaya damu kuna mafaza wengi na vijana, lakini ni kikosi
ambacho kinasemekana kukamilika zaidi, ndio maana kimeweza kuwapokonya
watani wao wa jadi mwari wa ligi hiyo.
Wakati
Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Oscar Samwel Joshua, Nadir Haroub
“Canavaro” wakisimama katika ukuta wa Yanga, vijana wa Simba, Haruna
Chanongo, Ramadhan Singano “Messi”, wakiongozwa na Mrisho Khalfan Ngasa
watakuwa wanatafuta maarifa ya kupenya na kumtafuta kipa nambari moja wa
Yanga aliyeitwa Taifa Stars na kukutana na mpinzani wake kwa mara
nyingine Juma Kaseja ambaye alimuweka benchi muda wote wakiwa Simba,
namzungumzia Ally Mustapha “Bartez”.
Katikati
ya dimba itakuwa burudani kubwa sana wakati Amri Athman Kiemba, Jonas
Mkude, Musa Mude, Mwinyi Kazimoto watakuwa wanapambana na akina Athman
Idd “Chuji”, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima “Fabrigas”, na Frank
Domayo.
Ngasa
ataichezea Simba mbele ya timu yake kipenzi ya Yanga, wakati akipangwa
kuongoza mashambulizi ya Simba akitokea winga ya kulia, kwa upande wa
Yanga, kijana mdogo anayehofia urejeo wa Ngasa jangwani, Simon Msuva
atakuwa anakimbiza upande wa kulia akipiga krosi ndani ya eneo la sebule
la Simba na kukutana na Didier Kavumbagu, Jerryson Tegete, Khamis Kiiza
“Diego” wanaotarajia kusimama sehemu ya mashambulizi.
Tayari maandalizi ya mechi hiyo ya watani wa jadi yamekamilika kwa mujibu wa viongozi wa timu hizo.
Afisa habari wa Yanga akiwa Pemba visiwani Zanzibar, Baraka Kizuguto ameimbia MATUKIO DUNIANI
kuwa wamefanya maandalizi mazuri na wanajipanga kuingia Dar es salaam
ili kutoa burudani katika mchezo wa kesho na kuibuka kidedea mbele ya
Mnyama Pori.
“Sisi
tumejiandaa vizuri ili kutoa burudani siku ya jumamosi, Yanga ni
mabingwa lakini hiyo haituzui kutafuta ushindi mbele ya wapinzani wetu
wakubwa katika soka la Tanzania, tuko fiti sana”. Alisema Kizuguto.
Kizuguto
alisema kwa kawaida kocha wao Mholanzi Ernie Brandts siyo msemaji sana,
ni mtu wa vitendo na ndio maana muda wote anashughulikia mazoezi
kujiandaa na mchezo huo.
“Kwa
mtu anayemfautilia kocha wetu, siyo msemaji sana ila ni mtu wa vitendo,
amekiandaa kikosi kwa uzuri, mashabiki wa Yanga waje kwa wingi
kushuhudia kikosi chao kilichotwaa ubingwa kikiwaadabisha Simba kesho”.
Alitamba Kizuguto.
Akizungumzia
hali ya wachezaji, Kizuguto alisema wachezaji wapo salama, hakuna
majeruhi mpaka sasa ambaye yuko hatarini kuwakosa Simba na wana morali
kubwa sana kuwakabili Simba hapo Kesho.
Alipoulizwa
timu itawasili lini Dar es salaam, Kizuguto aligoma kueleza akidai
Mechi za watani wa jadi huwa zina na fitina nyingi, lakini timu
itakuwepo jumamosi uwanja wa taifa. MATUKIO DUNIANI imebaini kuwa Yanga itawasili leo Dar es salaam na hii ni kwa mujibu wa kiongozi kigogo wa Yanga.
Wakati
Yanga wakijinasibu kuibuka na ushindi, Simba kwa upande wao wamesema
wapo tayari na wanasubiri kuwakabili wapinzani wao hapo kesho.
Mjumbe
wa kamati ya usajili, mjumbe wa kamati ya utendaji, na mratibu wa timu
katika mashindano, keptein wa zamani wa jeshi la kujenga taifa JWTZ ,
Zacharia Hans Poppe ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa wamekamilika na vijana wao wapo tayari kuwakabili wanaowaita wakongwe wa Yanga.
“Siku
inawadia, kesho siyo mbali jamani, njooni uwanja wa taifa ili muone
kazi yetu, wakati wa maneno umekwisha”. Alisema Poppe.
Poppe
alisema Simba bado wana wasiwasi mkubwa sana kufuatia TFF kubadilisha
mwamuzi wa mchezo bila taarifa yoyote kwao, ila wameshaandika barua
kwenda shirikisho wakiwataka waeleze sababu za kumuondoa Israel Nkongo
na kumuweka Saanya wa Morogoro katika kipute hicho.
“Wenzetu
toka mwanzo walikuwa wanamtaka mwamuzi huyo na wamempata, tutacheza
kulingana na ufundi wetu na mambo yatakwenda salama”. Alisema Poppe.
Pia
aliongeza kuwa mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi hata kidogo, kikosi
kipo shwari na vijana wao wana morali kubwa ya kuwanyoa Yanga bila
kutia maji hapo kesho.
Mzunguko
wa Kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara, miamba hiyo ilitoka sare ya
bao 1-1, lakini kilio bado kipo kwa Yanga ambao msimu uliopita walipigwa
kipigo cha aibu cha mabao 5-0.
Miongoni
mwa wachezaji walioongoza kikosi cha simba kuwafunga Yanga walikuwa ni
Emmanuel Okwi, marehemu “Mungu amlaze mahala pema peponi), Patrick
Mutesa Mafisango, Ferlix Sunzu na nyuma alikuwepo Kelvin Yondan, sasa
Sunzu pekee ndio yuko Simba mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment