Kikosi cha Taifa stars
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26
mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na
kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa
ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake
kipa Juma Kaseja.
Timu
hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi
ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya
wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Mbali
ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho
ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni
Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa.
Wengine
ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi
Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum
Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya,
Athuman Idd na Haruni Chanongo.
Wachezaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars
jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada
ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko.
Katika
msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim
Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred
Chimela (Mtunza vifaa).
0 comments:
Post a Comment