Thursday, May 23, 2013

DR WATOTO 059 bMkurugenziwahospitaliya IMTU Dkt. Ali Mzige akisitiza umuhimu wa wazazi kujali afya za watoto na kufuatilia uzito wa watoto wao walio chini ya umri wa miaka mitano alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Kulia kwake ni Bw.Saibal Sarbadhikari Meneja Mkuu wa umoja wa BANGO SANGHO.
DR WATOTO 064 bMkurugenzi wa hospitali ya IMTU Dkt. Ali Mzige akihamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la upimaji afya bure kwa watoto walio chini ya miaka mitano,utakaofanyika jumapili Mei 26 katika hospitali hiyo iliyopo Mbezi Beach. Kushoto kwake ni Bw.Saibal Sarbadhikari Meneja Mkuu wa umoja wa BANGO SANGHO.
Na Genofeva Matemu -MAELEZO
HOSPITALI ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Tekinolojia (IMTU hospital) kwa kushirikiana na Umoja wa Jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo nchini Tanzania watatoa huduma ya upimaji afya bure jumapili Mei 26 mwaka huu  kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaoishi maeneo ya Mbezi Beach .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa hospitali ya IMTU Dkt. Ali Mzige alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na afya ya mtoto na umuhimu wa maziwa ya mama hasa kwa watoto walio chini ya miezi 6 .
Dkt. Mzige amesema wanakusudia kupima uzito, presha na kutazama afya ya kinywa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambapo watatumia vifaa maalumu vya upimaji presha kwa watoto hao.
“Tutapima uzito ambao takwimu zake ni Kg 10 kwa mtoto wa mwaka mmoja, Kg 11 kwa mtoto wa mwaka mmoja na nusu, Kg 12 mtoto wa miaka 2, Kg 13 kwa mtoto wa miaka miwili na nusu, Kg 14 kwa mtoto wa miaka 3, Kg 15 kwa mtoto wa miaka mitatu na nusu, Kg 16 mtoto wa miaka 4, Kg 17 mtoto wa miaka minne na nusu, na Kg 18 ni kwa mtoto wa miaka mitano”, amesema Dkt. Mzige.
Akirejea matokeo ya sensa ya mwaka 2012 Dkt. Mzige amesema matokeo hayo yalionesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka mitano hapa nchini wamedumaa, ambapo asilimia 16 wana uzito pungufu (Underweight) na asilimia 5 wamekonda (Marasmic) wako kwenye rangi nyekundu ya kadi za watoto za kliniki.
Aidha Dkt. Mzige ameishauri jamii kula lishe bora na kamili sababu lishe bora huanzia nyumbani hivyo ni jukumu la jamii kupata elimu  ya chakula bora na mlo kamili wenye kujenga afya bora kwa watoto.
Zoezi la upimaji wa afya kwa watoto limeanza rasmi mwaka huu na linatarajiwa kufanyika kila mwaka au mara mbili kwa mwaka kwa kushirikiana na uhisani wa Bango Sangho jamii ya wahindi wanaoishi hapa nchini  ambao wamekua wakitoa vifaa vya kupimia afya za watoto.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video