Na Immaculate Makilika- Dodoma
SERIKALI
yawashukuru wafugaji wote nchini kwa mchango wao mkubwa
unaoliwezesha Taifa kutoagiza nyama toka nje ya nchi na badala yake
kuliingizia kipato kutokana na mauzo ya mifugo hai na nyama nchi za
nje.
Hayo
yamesemwa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
, Benedict Ole Nangaro ,wakati wa kipindi cha maswali na majibu, hata
hivyo Naibu Waziri huyo alisema kwamba mwaka 2011/2012, ng’ombe
3,362 na mbuzi/kondoo 4,060 wenye thamani ya Sh. Bilioni 3.81 waliuzwa
nje.
Aidha
tani 31.6 za nyama ya ng’ombe ,tani 647 za nyama ya mbuzi na tani
151.8 za nyama ya kondoo ziliuzwa nje na kulingizia Taifa takribani Sh.
bilioni 19.3
Fedha
iliyookolewa kwa kutoagiza nyama kutoka nje haiwekwi kama akiba
mahsusi bali hutumika kwa maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta
ya mifugo.
Nchi
yetu inajitosheleza kwa mahitaji ya nyama ambayo kwa mwaka tunazalisha
wastani wa tani 462,686, kwa mchanganuo wa nyama ya ng’ombe tani
248,108, nyama ya mbuzi/kondoo tani 92,351, nyama ya nguruwe tani 39,676
na nyama ya kuku tani 82,551.
Hata
hivyo, kutokana na mahitaji ya soko hususani wageni toka nje ,baadhi ya
hoteli za kitalii na migodi huagiza tani 800 za nyama maalumu kwa mwaka
,kiasi kinachogharimu Sh. bilioni 10.2.
Serikali
inaendelea kuwahimiza wafugaji kufuga kibiashara na kuzalisha nyama
bora ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ikiwemo migodi.
0 comments:
Post a Comment