NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA
WADAU wa kahawa wameziomba halmashauri kutenga kiasi cha fedha katika
mapato yao kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha kahawa kuliko kuendelea kudorora
siku hadi siku kutokana na wakulima wengi kutoona faida yake.

Waliyasema hayo jana wakati wakizungumza katika mkutano
uliwashirikisha wadau wa kahawa kutoka kanda ya kaskazini uliofanyika
mjini hapa na kuandaliwa na bodi ya kahawa Tanzania, uliolenga kujadili jinsi ya kuboresha zao hilo na kujiandaa kwa ajili ya mkutano mkuu wa wadau wa kahawa utakaofanyika may 30 hadi 31 mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkulima aliyejitambulisha kwa jina la
Lemburis Sirikwa alisema kuwa , zao hilo limedorora sana kutokana na wakulima wengi waliokuwa wakilima zao hilo kubadilisha matumizi ya mashamba na kulima kilimo kingine
kutokana na kutoona faida yake.

Sirikwa alisema kuwa, biashara ya kahawa hapa nchini imeporomoka kwa asilimia 90
kutokana na kuwa wakulima wengi wa kahawa wamekuwa wakiishia kupata hasara siku
hadi siku kutokana na zao hilo kutothaminiwa na serikali na kulichukulia uzito
kama mazao mengine yalivyo.

” Lazima halmashauri zijikite katika kufufua zao hilo la kahawa
katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku za dawa za pembejeo ili kuwezesha wakulima hao kutotumia gharama nyingi katika uandaaji wa mashamba na mwishowe kuishia kupata hasara kutokana na kutokuwa na masoko ya uhakika”alisema Sirikwa.

Naye Mkurugenzi wa maendeleo ya kahawa na uendeshaji bodi ya kahawa Tanzania ,
Godluck Sipira alisema kuwa, wameweza kukutana na wadau mbalimbali wa kahawa na
kuweza kusikiliza changamoto zao ambapo wameweza pia kutoka na
maazimio ambayo watayawasilisha katika mkutano mkuu wa wadau wa kahawa
na kuyajadili na hatimaye kuyatolea utatuzi.

Sipira alisema kuwa,lengo ni kuhakikisha kuwa sekta nzima ya kahawa nchini
inaendelezwa na kuweza kufufua zao la kahawa ambalo limeonekana kudorora katika
maeneo mbalimbali hapa nchini kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili
wakulima .

Aliongeza kuwa,ili zao hilo liweze kurudi kwenye hali yake ya kawaida
ni wajibu wa kila mdau kujitahidi kutekeleza wajibu wake kwa nafasi yake katika kutumia
rasilimali zilizopo katika kuhakikisha sekta ya kahawa inaimarika,na kusonga mbele katika kuleta tija ya kahawa.
Naye mkuu wa wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munasa aliitaka serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa kahawa kuhakikisha kuwa wanaandaa
utaratibu wa kuwapimia mashamba ya kahawa wakulima wa vijijini ili
kuweza kupata hati miliki na kuweza kupata mikopo katika mabenki na
taasisi mbalimbali za kifedha.

0 comments:
Post a Comment