Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Wadau wa elimu wametakiwa kutoa
ushirikiano wa dhati kwa taasisi za sekta hiyo kwa minajili ya kuboresha hali
ya elimu hapa nchini.
Mwenyekiti wa mfuko wa kijamii wa
walimu TGTF bwana Ephraim Mwikuka alisema mazingira ya
sasa ya elimu yana changamoto kubwa kwa upande wa waalimu na wanafunzi hivyo
kuhitaji nguvu za pamoja kuzitatua.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa TGTF
imejipanga kushirikiana na serikali na jamii katika kuboresha mazingira ya
elimu ya msingi na sekondari hapa
nchini.
Bwana Mwikuka amewataka watanzania
kuacha kulalamika bali wachukue hatua
katika kukabiliana na taasisi,jumuiya na serikali kwa ujumla kutatua
changamoto za kielimu katika jamii.
0 comments:
Post a Comment