Monday, May 20, 2013


Airtel-Rising-Stars-Pan-African-tournament Airtel Rising Stars
Viongozi wawili kutoka Manchester United — Anthony Benerjee,
Mkurugenzi wa Uhusiano na Michael Higham, Meneja Uhusiano — wanatua
jijini Dar es Salaam Jumatano hii kufanya manzungumzo na viongozi wa
Airtel Tanzania namna bora ya kuendesha michuano ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amesema mkutano huo
utakaojumuisha wadau mbalimbali utafanyika makao makuu ya Airtel
Tanzania jijini Dar es Salaam na kutathimini ARS ya miaka miwili
iliyopita ili kuona namna nzuri ya kuendesha michuano siku za usoni
kuanzia mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni moja ya wadau
wataoshiriki mkutano huo ili kutoa mchango wao hasa katika masuala ya
kifundi kama vile upangaji wa ratiba ya mashindano. Ratiba ya kuanza
kwa ARS 2013 inatarajiwa kutangazwa mwezi huu.
Michuano ya soka Airtel Rising Stars ilizinduliwa hapa nchini Tanzania
na sehemu nyingine barani Afrika mwaka 2011 ikiwa na lengo mahsusi la
kusaidia kuvumbua vipaji vya wanasoka chipukizi na kuwafanya waonekane
kwa makocha na mawakala wa kusaka vipaji vya wachezaji nyota.
Mashindano haya huanzia ngazi ya chini ambapo timu za sekondari ngazi
ya mkoa huchuana ili kupata wachezaji nyota wa kuunda kombaini
inayowakilisha mkoa husika kwenye mashindano ya Taifa ambayo hufanyika
jijini Dar es Salaam. Jumla ya timu 48 zimepata fursa ya kushirikia
ARS katika miaka miwili iliyopita.
Katika mwaka wa uzinduzi  2011 mashindano ya ARS ngazi ya Taifa
yalifuatiwa na kliniki ya kimataifa chini ya usimamizi wa makocha
kutoka Manchester United iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam na kushirikisha wavulana na wasichana kutoka nchi za
Kenya, Malawi, Sierra Leone na mwenyeji Tanzania..
Mwaka jana fainali za taifa za ARS zilifuatiwa na michuano ya
kimataifa ya ARS zilizofanyika jijini Nairobi zikishirikisha nchi
ambazo kampuni ya Airtel hufanya biashara. Vile vile kliniki ya mwaka
jana ilifanyika Nairobi chini ya usimamizi ya makocha wazoefu kutoka
shule za mafunzo ya soka ya vijana za Manchester United ambapo vijana
walipata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za soka.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video