Na Beatrice Mlyansi Maelezo
WAZIRI
wa ulinzi na Jeshi la kujengaTaifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha amewataka
viongozi wa dini nchini kuwa makini na kauli wanazotoa kwa waamini wao
kwani zinaweza kuleta madhara makubwa.
Nahodha
ameyasema hayo jana jijini Dar es saam katika kongamano la siku mbili
na viongozi wa dini ili kujadili mstakabali wa ulinzi na usalama nchini.
Waziri
Nahodha ameeleza kuwa kuwepo kwa dini mbili za Kikristo na Kiislamu sio
mzigo bali kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hizo kusema vibaya
dini nyingine ndio tatizo.
“Kuwepo
kwa dini hizi mbili hakuwezi kuwa mzigo,tatizo ninaloliona ni kauli
zinazotolewa na abaadhi ya viongozi, inabidi tuwe makini na wa kweli
maana wakati mwingine matendo yanasema zaidi”.Alisema waziri Nahodha.
Alisema
viongozi hao wanatakiwa kuwa makini sana kwani kauli moja inaweza
kutafsiriwa vibaya na upande mwingine bila kukusudia au la.
Waziri
ametaka viongozi hao wadini wajifunze kupitia waasisi wa imani zao
Bwana Yesu Kristo na Mtume Muhamad ambao walifundisha bila kukashifu
imani nyingine pamoja na mwanafalsafa Confucias ambaye alisisitiza watu
mwenye busara kutobadili misimamo yao kwenye masuala yenye maslahi ya
muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment