Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
wa watukutu wa London, Tottenham Hospur, Mreno Andre Villas-Boas bado
ana imani kubwa kuwa nyota wake na mfumania mabao wa klabu hiyo Gareth
Bale atabaki White Hart Lane msimu ujao licha ya klabu hiyo kushindwa
kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya.
Villas-Boas
amesema nyota huyo anakodolewa macho na timu nyingi sana ili kumsajili,
lakini bado Bale anaipenda Spurs na atabaki kuisaidia timu hiyo msimu
ujao wa ligi kuu nchini Uingereza ambao Manchester United watakuwa
wanatetea kombe lao chini ya kocha mpya David Moyes.
“Nilifikiri
kuwasaidia Spurs kucheza UEFA msimu ujao, sijafanikiwa, nawashauri
kusajili wachezaji wengine kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao. Ni
muhimu sana kumshawishi Bale abaki ili timu iwe bora zaidi”. Alisema
Bale.
Boas aliongeza kuwa ni ngumu sana kumuachia mchezaji mwenye uwezo mkubwa kiasi hiki, lazima timu imng`ang`anie kwa nguvu zote.
Tottenham
wamemaliza katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 72 huku washika
bunduki wa London wakimaliza nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 73,
lakini wamekata tiketi ya kucheza ligi ya Uropa msimu ujao.
Bale
alifunga bao lake la 26 msimu huu katika mchezo wa jana dhidi ya
Sunderland ambapo walishinda bao 1-0 lakini haijawasaidia kufuzu UEFA.
Miamba
ya soka la Hispania, Real De Madrid waliomaliza msimu huu bila kikombe,
mabingwa wa ligi kuu England, Manchester United na mabingwa wa
Bundesliga, wekundu wa kusini mwa Ujerumani, FC Bayern Munich
wanahusishwa na mbio kali za kuitaka saini ya nyota huyo.
Msimu wa ligi uliomalizika jana, Bale alishinda tuzo mbili, moja ya mwanasoka bora wa FA na mchezaji bora chipkizi.
Gareth Bale alifgunga bao muhimu hapo jana dhidi ya Sunderland na kuipa Spur nafasi ya kucheza ligi ya Uropa msimu ujao
KWA KUJIAMINI: Meneja wa Spurs Andre Villas-Boas anaamini Bale atabaki White Hart Lane
Wakati
huo Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy, ameandika taarifa yake ya mwaka
kwa mashabiki na kuchorea majina ya baadhi ya nyota wao anaotamani
kuwabakisha akiwemo Bale.
“Msimu
huu tunahitaji kuboresha kipindi, tutaendelea kufanya juhudi ya kufanya
hivyo na safari hii tunawabakisha wachezaji muhimu kwetu”. Alisema Levy
katika taarifa yake.
UNATANIA:
Wachezaji wa Spurs wakimshangaa mwamuzi wa jana Andre Marriner
aliyewanyima penati na kumuonesha kadi ya njano mchezaji Bale kwa madai
ya kumdanganya mwamuzi
Walifurahi sana lakini matokeo ya Arsenal yaliwaharibia nafasi yao ya UEFA na sasa watacheza ligi ya Uropa.
0 comments:
Post a Comment