Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Hakuna kushangaa hapa!!
Fainali
ya UEFA mwaka huu katika dimba la Wembley ni wajerumani tu, wekundu wa
kusini mwa nchi hiyo Fc Bayern Munich na nyuki wa kaskazini mashariki
Borussia Dortmund.
Ilikuwa
burudani ya aina yake katika dimba la Camp Nou nchini Hispania ambapo
FC Barcelona walikuwa wanahitaji ushindi wa mabao matano kwa bila dhidi
ya Munich baada ya kufungwa 4-0 katika mchezo wa kwanza, halafu
wakaambulia kipigo cha pili tena cha mabao 3-0.
Kikubwa
ambacho kinasemwa leo baada ya kipute hicho ni kuwa bila Messi timu
yoyote ingekuwa na hofu, hicho ndicho kilichowapata Barca jana hata kama
Xavi na Andres Iniesta walikuwemo ambao ndio mhimili mkubwa wa kikosi
hicho cha wakatalunya.
Leo
hii kocha wa Barca Tito Vilanova alijitetea kwa kitendo chake cha
kumchezesha Messi katika mchezo wa ligi kuu Hispani wikiendi iliyopita
licha ya kuwa na maamivu ya msuli wa paja, na hapo jana nyota huyo
alilazimika kukaa benchi kwa madai ya kuwa majeruhi.
“Alicheza
dhidi ya Bilbao ambapo tulitoka 2-2, alionekana kuwa vizuri lakini
mwishoni mwa mchezo alibadilika na kuonekana ana maumivu makubwa, jana
kulikuwa hakuna jinsi licha ya kumhitaji sana”. Alisema Vilanova.
Vilanova
aliendelea kusema kuwa hata ungekuwa na kikosi cha wachezaji wazuri
kiasi gani huwezi kushinda mataji yote, kufungwa kupo na wao wamekubali
kufungwa na wanadhani Bayern wako vizuri zaidi msumu huu.
Wembley tunaenda zetu: Arjen Robben (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Nou Camp jana
Soka larudi nyumabini kwao: Bayern na Dormund fainali mwaka huu
Lionel Messi (kulia) alikaa benchi licha ya timu yake kuhitaji ushindi wa mabao matano kwa yai ili kusonga mbele
VIKOSI
Barcelona:
Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra (Montoya 87), Adriano, Xavi (Sanchez
55), Song, Iniesta (Thiago 64), Villa, Fabregas, Pedro.
Subs: Pinto, Messi, Jonathan, Montoya, Tello.
Booked: Dani Alves, Pique
Bayern Munich: Neuer, Lahm (Rafinha 77), Boateng, Van Buyten, Alaba, Javi Martinez (Tymoschuk 74), Schweinsteiger, (Gustavo 66) Robben, Muller, Ribery, Mandzukic.
Subs: Starke, Dante, Shaqiri,Gomez.
Goals: Robben 49, Pique o.g. 72, Muller 76
Booked: Robben
Referee: Damir Skomina (Slovenia)
Watazamaji: 90,000
Subs: Pinto, Messi, Jonathan, Montoya, Tello.
Booked: Dani Alves, Pique
Bayern Munich: Neuer, Lahm (Rafinha 77), Boateng, Van Buyten, Alaba, Javi Martinez (Tymoschuk 74), Schweinsteiger, (Gustavo 66) Robben, Muller, Ribery, Mandzukic.
Subs: Starke, Dante, Shaqiri,Gomez.
Goals: Robben 49, Pique o.g. 72, Muller 76
Booked: Robben
Referee: Damir Skomina (Slovenia)
Watazamaji: 90,000
Gerard Pique (watatu kulia) aljifunga bonge la goli jana kipindi cha pili cha mchezo
Golikipa wa Barca, Victor Valdes akibwatuka baada ya Pique kujifunga
Mashabiki wa Barca walikuwa na matumaini makubw aya kuibuka na ushindi jana
0 comments:
Post a Comment