Na Gladness Mushi Arusha
ZAIDI ya vijana 80 kutoka hapa
nchini wanatarajiwa kunufaika na mradi maalum wa mfuko wa kuwasomesha
masomo ya ikolojia,mazingira na kufanya utafiti mradi utakaogharimu
kiasi cha shilingi milioni 400 .
Akizungumza na gazeti hili meneja wa utafiti katika chuo chaUniversity
times training Insititute Norah Isack alisema kuwa vijana hao wataanza
kunufaika na mradi huo hivi karibuni.
Alisema kuwa vijana hao watanufaika na mradi huo kupitia ushirikiano
baina ya chuo hicho na mashirika mbali mbali yaliyoko nchini marekani
lengo likiwa ni kuhakikisha vijana wa kitanzania nao wanakuwa mstari
wa mbele kufanya taffiti mbali mbali zikiwemo za uhifadhi wa wanyama
pori.
“kwa sasa najiandaa kwenda nchini marekani kwa ajili ya kufuatilia makubaliano baina yetu na mashirika ya kule marekani ya kuhakikisha kuwa hawa vijana wa kitanzania wanapata masomo ya tafiti mbali mbali
ambapo kupitia mafunzo haya yatasaidia kwa kiasi kikubwa hata kutoa ajira kwa vijana wetu”alisema Norah
Alieleza kuwa kwa sasa kumekuwepo na migogoro kati ya binadamu na wanyamapori kutokana na matukio ya uvamizi na uuwaji wa mifugo hivyo kupitia mafunzo hayo watayakayoyapata vijana hao yatapunguza
miggogoro hiyo.
Aliongeza kuwa mradi huo pia utaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa hata kuiokoa Tanzania hata kutoka kwenye orodha ya wanane hatari ambao wamekuwa wakiathiri wanyama pori kwa kuwa kupitia mafunzo hayo wataweza kujua namna ya kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori ambao wamekuwa
wakiathiriwa na baadhi ya watu.
Hata hivyo aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika utafiti wa utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa wanayam pori ili waweze kunufaika na mfuko huo maalum ambao utawawezesha kujikwamua
kiuchumi.

0 comments:
Post a Comment