Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Tawi
la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo
asubuhi ,(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk.Salim Ahmed
Salim.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa Kitaalamu
wa Chuo cha Ardhi serikali ya Muungano Dk.Staulans Ntiyakunze,(wa tatu
kulia) baada ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo asubuhi ,(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia meza na vikalio vyake wakati
alipotembelea moja ya madarasa katika Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo, baada ya kuzindua Chuo
hicho,(kushoto) Mkuu wa Chuo Dk. John Magoti, na pili kulia makamo wa
kwanza wa Rauis wa Maalim Seif Sharif,akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi

Mwalimu wa Darasa la Kompyuta Julius Maungo,akitoa
maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea katika darasa la kompyuta leo baada
ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko
Bububu Zanzibar leo asubuhi ,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea katika darasa la kompyuta leo baada
ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko
Bububu Zanzibar leo asubuhi ,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Dk. John
Magoti, baada ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo asubuhi alipotembelea sehemu
mbali mbali za Chuo hicho,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Baadhi ya wanafunzi wa Chu cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere Tawi la Zanzibar wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa chuo hicho
leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Nyerere Tawi la Zanzibar wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa chuo hicho
leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea zawadi kutooka kwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo cha Mwalimu Nyerere Dk.Salim Ahmed Salim,wakati wa uzinduzi
wa Tawi la Chuo hicho uliofanyika leo huko Bububu Nje ya Mji wa
Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Na Maelezo Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
ameitaka Bodi na Menejiment ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
kuendelea na jitihada za kukiimarisha Chuo hicho ili kutoa Elimu bora
yenye viwango vya kitaifa na kimataifa.
Rais
Shein ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Tawi la Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalim Nyerere lililipo Bububu nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
Amesema
njia nzuri ya kupelekea kiwango cha ubora wa elimu chuoni hapo ni
kuhakikisha Wanafunzi wanaojiunga wanakuwa na sifa zinazotakiwa pamoja
na kupata Walimu wenye ujuzi.
Ameongeza
kuwa ubora wa Elimu unaotolewa Chuoni hapo utawafanya Wahitimu
kukabiliana na ushindani wa Soko la Ajira jambo ambalo litaweka heshima
ya Chuo hicho.
Aidha
Dkt. Shein ameitaka Bodi ya Chuo kuandaa mikakati ya kuliwezesha Tawi
la Chuo hicho kuwa Chuo kamili kinachojitegemea badala ya kubakia kuwa
Tawi.
Amesema
Utaratibu wa aina hiyo ndio unaofuatwa Duniani kote ambapo Matawi ya
Vyuo vya Elimu ya Juu huwa yanaendelezwa na kuwa Vyuo kamili
vinavyojitegemea.
Dkt.
Shein amewataka Wanafunzi wa Chuo hicho kuitumia fursa waliyoipata ya
kuwepo Chuoni hapo kwa kujikita zaidi katika masomo bila ya kujiingiza
katika mambo yanayowapelekea katika malumbano.
Amewasihi
Wanafunzi wa Chuo hicho kuendeleza maadili mema sambamba na kufuata
Mila na silka zinazoendana na utamaduni wa kitanzania.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Dkt. John
Magotti alielezea mafanikio ya Chuo hicho kuwa ni pamoja na kukamilika
kwa Jengo hilo ambalo lina uwezo wa kuwahudumuia wanafunzi katika ngazi
za Cheti, Stashahada na Shahada.
Aidha
alielezea changamoto zinazokikabili Chuo hicho kuwa ni pamoja na
upungufu wa Mabweni ya kulalia Wanafunzi na Idadi ndogo ya Wanafunzi
wanaojiunga na Chuo hicho.
Amewataka
Wanafunzi wenye sifa kujiunga na Chuo hicho na kuwataka Wazanzibari
wenye ujunzi kuomba nafasi za ajira ikiwemo ufundishaji ili kukifanya
Chuo hicho kuwa na sura ya kitaifa.
Awali
akimkaribisha Dkt. Shein Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Dkt. Salim
Ahmed Salim amewataka Vijana kuithamini Elimu wanayoipata Chuoni hapo
ili iweze kuwa Mkombozi wa maisha yao.
Jengo
la Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililopo Bububu
limegharimu Jumla ya Shilingi Bilioni 3.6 ambazo zimegharamiwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa Tawi hilo ni
kwa ajili ya Wanafunzi wa ngazi ya Cheti.
0 comments:
Post a Comment