MWENYEKITI
wa Umoja wa Wafanyabishara Walemavu Dares Salaam (UWAWADA), Mohamed
Kidumke amesema kama serikali haitawasaidia mikopo walemvu basi kuna
hatari baadhi ya watu hao wakaendelea kuwa ombaomba barabarani milele.
Wakizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kidumke alisema badhi
ya walemavu hao hawapendi kukaa barabarani na kuomba bali wamekuwa
wakifanya hivyo kutokana na kukosa njia za kujiingizia kipato.
Alisema
Umoja wao unania ya kuwaondoa walemavu wote wanaomba barabarani kwa
kuwaanzishia biashara ndogondogo lakini bado jitihada zao hizo
zinahitaji uungwaji mkono na serikali kwa kuwapatia mikopo nafuu
walemavu hao ili waweze kujikwamua.
“Wapatiwe
mikopo pia watengewe maeneo ambayo yatawezesha kukutana na wateja kwa
wingi kwa mfano maeneo wanayolenga ni kama vile kwenye vituo vya
daladala”alisema Kidumke.
Kidumke
alisema ni muda mrefu umoja huo uliuomba uongozi wa Halmashauri ya
wilaya ya Ilala kuwatengea maeneo ya kufanyia biashara lakini hadi sasa
uongozi huo haujatoa jibu.
Alisema
wakati mwingine viongozi hao wamekuwa wakichukuliwa na umoja huo kama
chanzo kimojawapo kinachokwamisha juhudi za maendeleo yao kwa
kutozipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment