NA MAGRETH KINABO- MAELEZO, DODOMA
WAZIRI
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa
utafiti wa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi ijulikananayo kwa jina la
TAMOVAC -01 katika mkoa wa Mbeya unaoendelea na imeonesha kwamba ni
salama na ina uwezo wa kusisimua mwili na kuzalisha viini kinga katika
dozi ndogo.
Alisema utafiti huo unaofanywa na Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu umewashirikisha watu 60.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma wakati Waziri huyo
akiwasilisha hotuba yake kuhusu Makadrio ya Mapato na Matumizi ya
fedha kwa mwaka 2013/2014 ya sh. 753,856,475,000 ambapo aliomba Bunge
lijadili kuidhinisha.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/2013 wizara
yake ilipanua huduma za kinga, matunzo na tiba kwa ajili ya huduma za
VVU/Ukimwi.
Vituo
vya kutolea huduma ya mantunzo na tiba vimeongezeka kutoka vituo 956
mwaka 2011 hadi kufikia 1,176. Jumla watu 1,135,348, wanaoishi na
VVU wameandikishwa kupata huduma za matunzo,kinga na tiba.
Hivyo
kati ya idadi hiyo wanaopata dawa za kupunguza makali ya VVU ni 663,884
na imeweza kutuoa huduma za wagonjwa wa majumbani kwa wanaoishi na VVU
239,298.
0 comments:
Post a Comment