Mahmoud Ahmad Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha magessa Mulongo ameviwataka vyama vya wafanyakazi
kuwachunguza waajiri wanao kiuka sheria za kazi kwa kuajiri kwa miezi
mitatu mitatu kwani wamekuwa wakiwaacha wafanyakazi kama walivyowaajiri
mwanzo bila ya mafao ya mwisho wa kazi tuwakatae waajiri wasiofuta
sheria za kazi natoa agizo kuanza kufanya uchunguzi kwa waajiri kama
hawa.
Kauli hiyo ameitoa kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi kwenye viwanja
vya kumbu kumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa na kusema kuwa wapo
waajiri wa aina hiyo wengi wasiojali maslahi ya wafanyakazi na mwisho wa
siku kuwaacha hawana mafao yeyote huko ni kuwaumiza wafanyakazi.
Mulongo
alisema kuwa kumekuwapo na wahitimu ambao wenye stashahada na Diploma
wamekuwa wakiongoza kwa utendaji mzuri wa kazi wakati wenye digrii
wakiwa hawana uzoefu na moyo wakuifanyakazi na kubaki kupiga fitna na
wakati wakiwa vyuoni walikuwa wakifuatilia siasa na kuacha kufuta
taaluma zilizowapeleka vyuoni humo.
“Ndugu
zangu wafanyakazi wenzangu Taaluma yeyote inahitaji muda mzuri wa
kuifuatilia tangu ukiwa chuoni hadi unaingia kazini sasa hapa upo chuoni
unaacha taaluma unafuata mambo yasio ya taaluma huku ni kutokuwa na
wataalamu wa kufaa hapo ndipo fitna zinapoanzia”alisema Mulongo.
Mulongo
alienda mbali na kuwataka wanahabari kuandika habari kufuatana na
taaluma zao na kuacha ushabiki wa kisiasa kwani taaluma ya uandishi wa
habari ni taaluma yenye weledi na ina miiko na maadili hapa ndugu zangu
tuelimishe jamii masuala ya kimaendeleo badala ya kijikita kwenye
masuala ya kisiasa zaidi na kuicha nchi ikielekea kwenye lingi la
vurugu.
“ipo
wakati mtajikuta mkiangukia kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma
mbali mbali kwani mtakuwa mmeacha taaluma na kuuvaa ushabiki wa kisiasa
hapo mtakuwa hamuitakii nchini yenu maendeleo bali mtakuwa mnaitakia
nchi yenu mabaya”alisema mkuu wa mkoa.
Sherehe
hizo zilienda sambamba na maandamano ya vyama vya wafanyakazi na
makampuni mbali mbali huku maonyesho ya magari yakitia for a hasa
kampuni ya Megatrade Investment watengenezaji wa Kiroba orgin na Kvant
Gin na Kiwanda cha Banana Ivestment Huku kwenye viwanda vya kutengeneza
nguo Kampuni ya AtoZ ikitia for a ikifuatiwa na kampuni ya Sunflag zote
za jijini hapa.
0 comments:
Post a Comment