Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
mkuu wa mabingwa wa soka nchini Hispania, wazee wa Katalunya, FC
Barcelona, Tito Vilanova ameondoka leo kwenda jijini New York nchini
Marekani ili kupata matibabu zaidi ya ugongwa unaomsumbua, saratani ya
ini.
Tito
alitakiwa aende baada ya msimu kumalizika, lakini klabu imeamua
kumpeleka wiki ijayo kwani tayari FC Barca imeshatwaa kombe la La Liga.
Vilanova atakaa Marekani kuanzia leo hii mpaka ijumaa akipata matibabu zaidi nchini humo.
Vilanova
alishindwa kuiongoza Barca kwa wiki sita msimu huu baada ya kukaa
katika matibabu mapema mwaka mwaka huu, lakini mechi ya mei 29 atakuwa
Hispania na kuiongaza klabu yake mbele ya Espanyol.
Vilanova
mara nyingi amelaumiwa kwa upangaji wa kikosi chake hususani katika
michuono ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Bayern Muinich ambapo
mchezo wa kwanza walifungwa mabao 4-0 uwanja wa Allianz Arena na mechi
ya marudiano Camp Nou wakachapwa 3-0 na kutolewa kwa wastani wa mabao
7-0.
Katika
mechin ya Marudiano Vilanova alimuweka benchi nyota wake Lionel Messi
na kuzua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wengi wa kandanda duniani.
MATIBABU: Bosi wa Tito Vilanova ameondoka leo kwenda Marekani kupata matibabu zaidi
WAKIWA
KATIKA BASI LAO: Vilanova na msaidizi wake Jordi Roura (kushoto), na
kocha wa mazoezi ya viungo Juanjo Brau (kulia) wakiwa katika basi la
Baraca siku ya kushangilia ubingwa wao huku mashabiki wao wakijipanga
katika barabara za mji wa katalunya
0 comments:
Post a Comment