Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya Hipop Ney wamitego akitumbuiza katika moja ya matamasha ya Airtel yatosha
Msaniii wa Miondoko ya Hip Hop ROMA Mkatoliki akitoa burudani wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha
- Ney, Nuture, Roma, Madee, na Fid Q kupamba jukwaa la Airtel yatosha BURE
Katika
mfululizo wa matamasha ya Airtel Yatosha yanayoendelea mikoa mbalimbali
nchini , Kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki hii itatoa burudani
pamoja na utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wakazi wa temeke ,
jijini Dar es salaam katika viwanja vya Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi
na Jumapili ya tarehe 4 na 5 mwenzi May 2013.
Tamasha
la Airtel yatosha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi
kipya wakiwemo , Sir Juma Nature akiwa na kundi la wanaume halisi,
Madii akiwa na kundi zima la tiptop connection, pamoja na wakali wa
hipop Fid Q , Roma Mkatoliki na Ney wa mitego
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando
amesema, tumefanya matamsha ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali
nchini lengo hasa likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma zetu ikiwemo
Airtel yatosha na kuwaunganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano
bora na bei nafuu wa Airtel,
Na
mwishoni mwa wiki hii tunawafikia wateja na wakazi mkoa wa Dar es
salaamawa na kuwapa nafasi ya kusajili namba zao, kujiunga na huduma ya
Airtel yatosha, Airtel Money na internet ya kasi ya 3.75G, kupata
elimu kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Airtel na kuunganishwa na
mtandao wa Airtel kwa wale wateja wapya.
Kiingilio
ni BURE, Njoo na kitambulisho chako upate kuunganishwa na huduma zetu
na kupata burudani kutoka kwa wasanii mahiri wa kizazi kipya Aliongeza
Mmbando.
Kujiunga
na huduma ya Airtel Yatosha mteja anatakia kupiga *149*99# na
kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua
kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe
mfupi na kifurushi cha internet.
0 comments:
Post a Comment