Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji
noyta na mzee wa matukio wa klabu ya Liverpool Luis Suarez amesema sasa
ni wakati muafaka kwa yeye kuondoka lakini hajafanya uamuzi wowote
kuhusu nini afanye baadae.
Suarez,
Miaka 26, ambae kwa sasa yupo kwenye Adhabu ya kufungiwa Mechi 10 kwa
kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, amekiri ni vigumu kuikataa
Real Madrid huku kukiwa na uvumi wa yeye kuunganishwa na kuhamia Klabu
hiyo.
Amesema: “Ni wakati muafaka kubadilisha mazingira kwa sababu ya yale yaliyonitokea huko England. ”
Suarez:
-Goli 30 kwa Mechi 44 alizochezea Liverpool Msimu wa 2012/13
-Tangu ajiunge Liverpool kutoka Ajax Januari 2011, amefunga Goli 51 katika Mechi 96.
-Alifunga Bao 49 katika Mechi 48 alizochezea Ajax kabla kujiunga Liverpool
-Amefunga Bao 31 kwa Mechi 62 alizochezea Uruguay
MZEE WA MATUKIO: Suarez yuko mbioni kusepa zake kuelekea Real Madrid
Suarez Aliongeza: “Sijui wapi nitakwenda na sijui kama nitabaki!”
Suarez,
ambae pia alifungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Beki wa Manchester
United Patrice Evra Mwaka 2011, aliongeza: “Ni wajibu kuishukuru Klabu,
na Mashabiki wa Liverpool. Lakini kwa jinsi ninavyotendewa na waliobaki
huko England imefanya Wiki hizi zilizopita kuwa ngumu. Liverpool ni
Klabu ya ajabu lakini wanajua jinsi ninavyotendewa na Vyombo vya
Habari!”
Suarez
alijiunga na Liverpool kutoka Ajax Mwaka 2011 kwa Dau la Pauni Milioni
22.7 na Msimu uliopita alifunga Bao 30 lakini alizikosa Mechi mbili za
mwisho za Ligi alipoanza kutumikia Kifungo chake cha Mechi 10 kwa
kumuuma Ivanovic.
NYOTA MWENYE MATUKIO: Suarez ametia kambani mabao 23 katika mechi 33 alizocheza msimu uliopita
0 comments:
Post a Comment