Imehamishika kutoka kwa Bin Zubeiry, Rabat
Amepunguza dozi; Stewart Hall |
Na Jaffar Iddi, Rabat
KOCHA wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall leo amepunguza dozi ya mazoezi kuelekea mchezo wa marudiano, Raundi ya Tatu Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, AS FAR Rabat utakaopigwa keshokutwa mjini hapa.
Jana, Stewart aliwafanyisha mazoezi mara mbili wachezaji wake kwenye viwanja vya michezo Rabat asubuhi na jioni, baada ya juzi kufanya mara moja.
Akizungumza na leo baada ya mazoezi ya mchana Uwanja wa maeozi wa wenyeji wao, FAR Rabat, Stewart alisema ameamua kupunguza dozi ili kuepuka kuwachosha wachezaji wake kabla ya mechi.
“Juzi tumefanya mazoezi magumu mara moja, jana pia mara mbili. Leo tumefanya mara moja tu. Na kesho tutafanya mara moja Uwanja ambao tutachezea mechi, tena katika muda wa mechi,”alisema.
Stewart alisema maandalizi yanaendelea vizuri na vijana wako vizuri kuelekea mchezo huo. “Kila kitu safi,”alisema.
Azam iliwasili hapa Jumatatu baada ya safari ndefu ya takriban saa 14 angani na saa mbili na ushei barabarani- saa tano kutoka Dar es Salaam hadi Dubai na saa tisa kutoka Dubai hadi Cassablanca- kisha saa mbili kwa barabara hadi Rabat.
Iliondoka Dar es Salaam Jumapili saa 11:00 jioni na kufika Dubai saa 6:00 ambako ililala hadi asubuhi ya jana ilipoondoka kuja Morocco na wachezaji walifika wamechoka kwa uchovu wa safari ndefu.
Ikumbukwe, Azam inayoshiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Afrika, inahitaji sare yoyote ya mabao au kushinda, ili kusonga mbele, baada ya awali katika mchezo wa Dar es Salaa kulazimishwa sare ya bila kufungana.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdallah hapa Rabat, wenye uwezo wa kukusanya mashabiki 52,000 kuanzia saa 11:00 kwa saa za hapa, sawa na saa 1:00 kwa saa za nyumbani, Tanzania.
0 comments:
Post a Comment