Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya pamoja na viongozi wengine wa
chama na Serikali pamoja na wadau mbali mbalimbali na wafanyakazi
wakiimba wimbo wa wafanyakazi maarufu kama “Solidarity Forever” Katika
viwanja vya sabasaba mjini Namanyere Wilayani Nkasi zilipofanyika
sherehe hizo kimkoa jana. Kauli mbiu ya sherehe hizo za Mei Mosi mwaka
huu ni “KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI”
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi
Ndugu Iddi Hassan Kimanta wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa
yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe
za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana.
Maonesho ya wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi kwa vitendo ilinogesha sherehe hizo.
Maandamano
ya wafanyakazi na mabango yenye jumbe mbalimbali ilikuwa sehemu ya
maadhimisho hayo. Kauli Mbiu ya sherehe hizo kitaifa ilikuwa “KATIBA
MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI”
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka na Kaimu Katibu Tawala
Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashala wakiangalia maonesho mbalimbali
yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika
kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa
jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitetea jambo na Mkuu wa
Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta wakati wa maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi iliyofanyika kimkoa Wilayani humo jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi cheti na zawadi
mmoja ya wafanyakazi bora wa mwaka 2012/2013 katika Ofisi ya Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Elvira Malema ambaye Sekretari wa Mkuu huyo
wa Mkoa jana katika uwanja wa sabasaba Mjini Namanyere Wilayani Nkasi.
Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Hassan Kimanta.
Michezo
mbali mbali ya mpira wa miguu na netiboli pia ilifanyika ikiwa ni
kuhamasisha michezo kwa wafanyakazi kwa ajili ya kuboresha afya zao
kazini na kazi zao kwa ujumla. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa salam za Mei Mosi kwa wachezaji wa timu za
Veteran Sumbawanga na Namanyere Nkasi kabla ya kuanza kwa mpambano,
timu hizo zilitoa sare 1-1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi
Hassan Kimanta.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
0 comments:
Post a Comment