Serikali imeridhia
kutungwa kwa sheria ya Kusimamia vyombo vya Habari ambapo muswada wa
kutunga sheria hiyo utawasilishwa bungeni hivi karibuni.
Akisoma
hotuba ya bajeti ya Wizara yake bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alisema
baada ya sheria hiyo kupitishwa na bunge, Wizara itaanza kuandaa waraka
wa mapendekezo ya kutunga sheria ya Haki ya kupata Habari wakati
serikali ikiendelea na utafiti ili kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali
zenye sheria hii.
Kwa
mujibu wa Dkt. Mukangara kutungwa kwa sheria ya kusimamima vyombo vya
habari kutasaidia katika kuimarisha tasnia ya habari nchini na kupunguza
kwa kiasi kikubwa changamoto zinazoikabili wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo likiwemo suala la mafunzo kwa waandishi wa habari
pamoja na mazingira duni ya kazi.
Katika
hotuba yake Dkt. Mukangara alisema pia Wizara yake imeazimia kutekeleza
suala la uanzishwaji wa benki ya Vijana ya Taifa katika mwaka wa fedha
wa 2013/2014.
Aliongeza
kuwa Wizara pia itaboresha huduma ya Mfuko wa Maendeleo ya mikopo yenye
masharti nafuu kwa vijana pamoja na kuendelea kuzijengea uwezo SACCOS
zinazotoa huduma kwa vijana.
Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo inaomba kuidhinishiwa bajeti ya jumla ya
shilingi 21,328,045,000 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za matumizi ya
kawaida ni 20,728,045,000 na fedha za miradi ya maendeleo ni shilingi
600,000,000
0 comments:
Post a Comment