RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE |
Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakuu na wamiliki wa
shule na vyuo binafsi kwa minajili ya
kuboresha sekta ya elimu haoa nchini.
Akizungumza na viongozi wa TAMONGSCO Rais Kikwete amesema
sekta binafsi ina mchango mkubwa wa kuinua elimu hapa nchini hivyo jitihada za
pamoja zinahitajika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza.
Rais Kikwete aliwataka wamiliki na wakuu wa
shule na vyuo binafsi kupunguza ada kubwa wanazotoza kwa wanafunzi ili watanzania
wengi hasa wa kipato cha chini waweze kupata fursa ya elimu.
Aidha Mheshimiwa Rais
alisema serikali iko katika Mchakato wa kutunga Sera Mpya ya Elimu baada ya ile
ya mwaka 1995, umefikia katika hatua za mwisho na kinachosubiriwa sasa ni maoni
ya Wabunge ili Sera hiyo ikamilishwe na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta
ya elimu.
Wakati huo huo
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania itaanza
maandalizi ya kupitia upya mitaala ya elimu nchini ili nayo ilingane na malengo
ya Sera Mpya ya Elimu,mahitaji ya maendeleo nchini na duniani kwa ujumla.
Licha ya
changamoto zinazoikabili sekta ya elimu serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa elimu imeongeza sekta hiyo ambapo kuna wanafunzi zaidi ya milioni
nane katika shule za msingi,zaidi wanafunzi
milioni moja na laki nane kwa shule za
sekondari na zaidi ya laki moja na sitini elfu kwa upande wa vyuo vikuu.
0 comments:
Post a Comment