Na Immaculate Makilika- Maelezo
SERIKALI
imesema inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika
jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336 katika
barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia
takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la
Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.
Hayo
yalisemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge
Naibu wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Temeke Abasi
Zuberi Mtemvu lililouliza kuwa Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu
ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?
Alisema
kuwa inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza
msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni kama
ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni
–Morocco (Sh. bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa
haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).
Nyingine
ni Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh. bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa
(Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh. bilioni
35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya
Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani
(Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa
ajili ya ujenzi.
Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).
Waziri
huyo alisema ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka Morocco
kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari
kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.
Aliongeza
kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano na kujenga
barabara ya juu (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga daraja lingine
pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala (salender bridge
Bypass) kutokea Kenyata Drive kuunganisha na Ocean Road.
0 comments:
Post a Comment