Na Immaculate Makilika- Maelezo
SERIKALI
imesema kuwa imeandaa mkakati wa kuendeleza tasnia ya kahawa (
Tanzania Coffee Industry Development Strategy,2012-2022) kwa lengo la
kuendeleza kilimo cha zao hilo nchini kupitia Bodi ya kahawa nchini
na kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya hiyo.
Aidha
Serikali imefafanua kuwa hatua hiyo ni kuongeza uzalishaji ,tija na
ubora wa kahawa Kitaifa ili kuboresha mapato ya wakulima wa zao hilo
katika mikoa mbalimbali inayolilima ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro .
Kauli
hiyo ilitolewa leo Bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mahusiano na
Uratibu Steven Wassira kwa niaba Waziri wa Kilimo ,Chakula na Ushirika
, Chrisopher Chiza , wakati akijibu swali la Grace Kiwelu(Mbunge
Viti Maalum-CHADEMA) aliyeuliza Je,Serikali ina mpango gani madhubuti
na mahsusi wa kufufua kilimo cha Kahawa mkoani Kilimanjaro ambacho kwa
miaka mingi kimekua tegemeo kwa wananchi wa Kilimanjaro na mhimili
mkubwa kwa uchumi wetu wa Taifa letu.
Alisema
malengo mahsusi ya mkakati huo ni pamoj ana kuongeza na uzalishaji wa
kahawa safi kutoka wastani wa sasa wa tani 50,000 kwa mwaka hadi
kufikia tani 100,000 ifikapo mwaka 2022 na kuongeza ubora wake ili
kupata bei ya ziada katika masoko ya nje kutoka wastani wa asilimia 35
hadi kufikia wastani wa asilimia 70 ifikapo mwaka 2022.
Aidha
Wassira alisema maeneo muhimu katika mkakati huo ni pamoja na
kuimarisha huduma za ugavi ili wakulima wazingatie kanuni bora za
kilimo,kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa (TaCRI) ili
kuhakikisha upatikanaji wa miche bora ya kahawa ,pamoja na kuongeza
matumizi ya viwanda vya kati vya kuitayarisha ili kuongeza ubora wa zao
hilo na hivyo wakulima kunufaika na bei nzuri.
0 comments:
Post a Comment