Na Baraka Mpenja
Kocha
wa zamani wa Temeke Squad na Moro United “Chelsea ya Bongo” Hassan
Banyai amesema yupo katika mazungumzo na baadhi ya timu ambazo hakutaka
kuzitaja majina ili kupata timu ya kufundisha msimu ujao.
Banyai
ambaye alikuwa anaongeza kisomo cha ukocha alisema kuwa kwa sasa
anataka kupata timu nzuri ya daraja la kwanza au ligi kuu, na wakati
huu anazungumza na timu nyingi na baada ya kuridhika atatangaza klabu
gani ataifundisha.
“Kuwa
kocha kuna changamoto nyingi sana, lakini unatakiwa kujipanga vizuri na
kujiamini, mwangalie Mourinho licha ya kukabiliwa na changamoto bado
anajiamini sana, nafikiri kutumia akili hiyo mara nitakapoanza kazi
yangu”. Alisema Banyai.
Kocha
huyo aliongeza kuwa akipata timu ya kufundisha atafanya kazi kwa ustadi
ili kuendelea kuwajengea imani watanzania kuwa makocha wazawa pia
wanaweza kulipatia mafanikio taifa.
Banyai
ambaye alikuwa na Moro United msimu wa 2011/2012 alisema bado
watanzania hawana imani na makocha wazawa kama wanavyofanya wenzetu
hususani Wanigeria ambao walitwaa kombe la mataifa ya Afrika Mwaka huu.
“Ifike
wakati na sisi tuige mfano wa mataifa ya magharibi ambao kwa sasa
wamejenga imani na makocha wazawa, kama watanzania watawapa sapoti
makocha wao tutapata waalimu wazuri ambao wanaweza kufundisha hata nje
ya nchi”. Alisema Banyai.
Kocha
huyo aliyewahi kufanya kazi na Fred Ferlix Minziro akiwa kocha msaidizi
katika kikosi cha Temeke michuano ya Taifa Cup na baadaye kuwa kocha wa
timu ya mkoa wa Ilala alisisitiza kuwa hakuna kitu cha maana kama
kuwapa nafasi wazawa ingawa hata watu wa nje wana nafasi yake.
“Kwa
mfano kama timu ina kocha Mzungu basi wajitahidi kuweka wasaidizi wake
wote wawe Watanzania kuliko kuweka wazungu pekee”. Alisema Banyai.
Banyai
alisema kasumba ya kutafuta makocha wa nje ipo katika klabu nyingi za
Tanzania lakini uwezo wa kifedha ndio kikwazo na kama klabu zingekuwa na
uwezo sawa asilimia kubwa zingekuwa na makocha wa kigeni.
“Imebaki
kwa timu zetu kubwa Simba, Yanga na Azam ambazo kwa kiasi kikubwa zina
uwezo mkubwa wa kifedha, angalia makocha wakuu wote ni wazungu, lakini
naamini kuna makocha wa hapa nyumbani ambao wanaweza kufanya kazi nzuri
zaidi yao”. Alisisitiza Banyai.
Hakika
nabii haheshimiwa kwao, taifa likiiga mfano wa Nigeria, Tanzania
itakuwa kitalu cha kuzalisha makocha wenye ubora mkubwa katika mchezo wa
mpira wa miguu.
0 comments:
Post a Comment