Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji
hatari wa mabingwa wa soka nchini England, Manchester united, Wayne
Rooney hajasafiri na timu yake kuwafuata West Bromwich katika mchezo wa
mwisho wa kibabu leo hii kwa makubaliano na kocha wake aliyestaafu
kuifundisha United, Alex Ferguson.
Rooney amepewa rukusa ya kubakia kutokana na mke wake Coleen kuwa na uchungu wa kujifunga mtoto wa pili tangu usiku wa jana.
Wawili hao tayari wana mtoto wao wa kwanza mwenye umri wa miaka mitatu anayeita Kai.
Jumapili
ya leo (MEI 19) ndio tamati ya Msimu wa 2012/13 wa BPL, Barclays
Premier League, na tayari Bingwa ni Manchester United, Mshindi wa Pili
ni Manchester City na Timu 3 zinazoshushwa Daraja ni Wigan, QPR na
Reading, lakini bado Timu 2 za nyongeza, kuungana na Man United na City,
kwenda kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu ujao hazijapatikana na
kimbembe hicho kiko kwa Chelsea, Arsenal na Tottenham.
Hata
hivyo, Chelsea wanaonekana wako salama zaidi kwani ni Arsenal tu ndio
inaweza kuwapiku kwa Pointi wakati Tottenham wanachoweza kukifanya ni
kuifikia Chelsea kwa Pointi lakini kuwapiku ni kitu kigumu maana Chelsea
wana Tofauti ya Magoli 35 wakati Tottenham wana 19 tu.
BPL:
RATIBA-MECHI ZA MWISHO MSIMU HUU: Chelsea v Everton, Liverpool v QPR,
Man City v Nowrich, Newcastle v Arsenal, Southampton v Stoke, Swansea v
Fulham,Tottenham v Sunderland, West Brom v Man United, West Ham v
Reading, Wigan v Aston Villa
UBINGWA: Wayne Rooney msimu huu ameshinda taji la tano akiwa na Manchester United, je ataweza kushinda lingine?
Hatima
yaRooney kubaki OLD TRAFFORD itajulikana siku chache zijazo kufuatia
kuwepo kwa taarifa kuwa nyota huyo atakutana na kocha wake mpya David
Moyes kujadili suala lake.
Rooney
siku za karibuni amekuwa na mawazo kuwa kocha Sir Alex Fergusona
amekuwa akimtenga katika kikosi chake na akaomba aruhusiwe kuihama klabu
hiyo.
Matumaini
ya nyota huyo yamerejea baada ya kocha David Moyes ambaye ni kocha wa
zamani wa Everton kuonesha nia ya kutaka kumbakisha united.
Rooney na David Moyes wanatarajiwa kukaa ili kuzungumzia hatima ya Rooney
0 comments:
Post a Comment