Mwandishi Wetu
SHINDANO la mkutafuta malkia
wa Mkoa wa Tanga mwaka huu “Redd’s Miss Tanga 2013″ litafanyika Juni 22
kwenye Uwanja wa Mkwakwani,Mkoani humo.
Akizungumza na gazeti hili
jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, alisema
kuwa warembo tayari wameanza mazoezi yakatofanyika kwenye Ukumbi wa
Lavida uliopo jijini Tanga.
Kigundula alisema shindano
hilo litaanza saa 2, usiku, ikiwa ni pamoja na kuwa na burudani
mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa nchini pamoja na
wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo.
Kigundula alisema kuwa mpaka
juzi warembo 10 wamejitokeza na kuanza mazoezi yanayosimamiwa Miss Tanga
2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.
Hawa Ramadhan (18),Hazina
Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18),Waida Mmbwambo(20),
Tatu Hussein(19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida
Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21).
0 comments:
Post a Comment