MMOJA wa wachezaji nyota historia ya Real Madrid, Zinedine Zidane amepewa jukumua la kuhakikisha nyota wa Tottenham, Gareth Bale anatua Bernabeu kwa dau la Pauni Milioni 65.
Gazeti la Hispania, Marca limeripoti kwamba Galactico
huyo wa zamani, Zidane ni mshauri mkuu katika mpango wa usajili huo na
anajaribu kumshawishi Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwamba
saini ya Bale ni kitu pekee muhimu.
Kipaumbele namba 1: Gwiji wa Real na
Ufaransa, Zinedine Zidane (kushoto) na mchezaji anayewaniwa na klabu
nyingi Ulaya, Gareth Bale (kulia)
Mpiga debe: Zinedine Zidane amesema Gareth Bale ni zaidi ya bora kiasi cha kutosha kucheza Real Madrid
"Kitu ambacho kimenivutia kwa ujumla ni kwamba ana muendelezo wa ubora. siyo wa mechi moja au mbili.Zidane
ambaye anamzimikia kwa muda mrefu nyota huyo wa Wales, amesema:
"Nimekuwa nikiitazama Tottenham kwa sababu Gareth Bale amekuwa akicheza
huko. Mbali na Ronaldo na Messi, ndiye mchezaji ambaye amekuwa
akinivutia zaidi duniani. Ni wa uhakika,".
"Anaendeleza kufunga mabao mazuri na muhimu. Ni mwepsi sana, mwenye kipaji na anayevutia.
"Ndiyo, wachezaji wenye kipaji kama yeye
wanaweza kuja Real Madrid. Ni mzuri kiasi cha kutoha kwa Real Madrid?
Ndiyo. Ni zaidi ya mzuri kiasi cha kutosha kucheza Real Madrid.’
Zidane alikuwa mchezaji mtu muhimu
katika biashara ya usajili Madrid tangu astaafu mwaka 2006. Alichangia
mno kutua kwa Raphael Varane Bernabeu na ana matumaini ya kumleta Bale
katika njia ile ile.
Kivutio: Bale akiichezea Spurs. Amemvutia Zidane msimu huu
Baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, Bale ndiye mchezaji anayemvutia zaidi Zidane
0 comments:
Post a Comment