Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Watangazaji
wa mpira wa miguu utawasikia kwa maneno kama haya, “dakika zilizobaki
ni ngumu kuzitaja!, tunamuangalia mwamuzi tu!, ni nafasi ya mwisho kwa
Real Madrid, wakishindwa kufunga basi ndio hivyo wamekwenda na maji!.
Nini pale? Kocha Mourinho anazozana na mwamuzi pale, mwamuzi anasemaje”, heeee! kadi nyekundu! Kwa Mourinho!.
Ronaldo anafanya madhambi pale, haaa! mbaya sana ile, dhahiri shahiri mwamuzi atatoa adhabu, nini? eeeh! kadi nyekundu!
Hivyo
ndivyo usiku huu watangazaji wa soka walivyotangaza wakati Real Madrid
wakipoteza mchezo wa fainali wa Copa Del Rey dhidi ya Atletico Madrid
huku Ronaldo na Mourinho wakioneshwa kadi nyekundu.
Kazi
kwisha, kocha mwenye ngebe nyingi na maneno mengi zaidi duniani, Mreno
Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho hatimaye amemaliza msimu wa
2012/2013 bila kikombe chochote baada ya usiku huu kupoteza mchezo wa
fainali ya Copa Del Rey kwa kufungwa mabao 2-1 na wapinzani wake wakubwa
katika mji wa Madrid, klabu ya Atletico Madrid.
Bao
la dakika za majeruhi lililotiwa kambani na mchezaji wa Atletico Joao
Miranda limeipa ushindi wa 2-1 na kuacha machungu makubwa kwa benchi la
ufundi, wachezaji na mashabiki wa Real De Madrid ambao wamemaliza msimu
bila taji lolote huku wapinzani wao wakubwa FC Barcelona wakiwa
wameshatwaa ubingwa wa La Liga.
Katika
mchezo huo, dunia imeshangazwa na kitendo cha Kocha Mourinho kupewa
kadi nyekundu na mwamuzi Clos Gomez kufuatia kutoelewana lugha , huku
baadaye nyota wa klabu hiyo Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo naye
akioneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji Gab.

Msumari
wa Ushindi: Joao Miranda akitia kambani bao la pili na la ushindi kwa
Atletico Madrid watoto wa mjini wanasema amepiga ndosi ya maana
kuzamisha gozi kambani, si mchezo hiyo ndio kazi

Duuh! haamini kabisa: Haya ni kadi nyekundu kwa Cristiano Ronaldo, baada ya kumfanyia madhambi Gabi

Haya sasa!, ze spesho one: Mwamuzi Clos Gomez anamuonesha kadi nyekundu kocha wa Real Madrid Jose Mourinho

Ronaldo alikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongeza katika
dakika ya 55 na baadaye Diego Costa aliisawazishia Atletico Madrid
akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na nyota anayewindwa na Mmiliki wa
Chelsea ,Roman Abramovich ili amsajili msimu ujao, Radamel Garsia Zarate
Falcao.
Kipindi cha pili mchezo ulianza kwa Real Madrid kutafuta bao
la pili, lakini bunduki zao ziligonga mtambaa panya mara tatu na kuoshwa
kwa umakini mkubwa na walinzi wa Atletico.Bao la ushindi la Miranda limewapa ushindi wa kwanza wa nyumbani Atletico Madrid tangu mwaka 1996.

Bonge la msumari: Diego Costa akiisawazishia timu yake huku kipa Diego Lopez akiambulia manyoya tu!

Basi la Real Madridi liliingia uwanjani kwa ngebe nyingi huko wakilakiwa na mashabiki wao

Si mchezo!: Kocha wa Atletico Diego Simeone akishangila bao la timu yake

Mwari huyooooooooo!! wa The Copa Del Rey, Real Madrid wameishia kunawa, hakuna kumgusa jamani!

Jose Mourinho akiwa jukwaani akihesabu siku za kuwa kocha wa Real Madrid
Sasa itakuwa njia nyeupe kwa
Mourinho kuondoka Hispania na kurejea England huku ikisemekana
atakapotua Chelsea anataka kumchukua Ronaldo ili kuimarisha kikosi
chake, wakati huo Manchester United nao wanataka kumrejesha nyota wao
huyo wa zamani.

Ronaldo chini ya ulinzi mkali, hapiti mtu, bora mpira upite
0 comments:
Post a Comment