Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar
Mhe Andry Rajoelina wakati wa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam
jana Mei 3, 2013.
PICHA NA IKULU
Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jana jioni , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Amepokelewa
kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na
mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.
Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa
ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari mwaka huu.
Rais
Kikwete alipokutana mara ya mwsho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya
Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Rais
Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi Rais wa zamani wa
Madagascar Mhe Marc Ravalomanana asigombee katika uchaguzi mkuu huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
0 comments:
Post a Comment