Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Baada
ya kuvuliwa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya walioutwaa mwaka
jana, kukosa ubingwa wa England na kombe la FA nchini Uingereza,
hatimaye wazee wa London, klabu ya Chelsea wamefanikiwa kupunguza
machungu baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya Uropa usiku wa kuamkia leo.
Chelsea
wameifunga Benfica 2-1 katika mchezo wa fainali na shukuruni za pekee
ni kwa beki wake Branislav Ivanovic aliyefunga bao dakika ya lala kwa
buriani (Dakika 93) na kumpatia kocha wake wa muda Rafa Benitez
atakayeondoka baada ya msimu huu na kumpisha kocha mwingine
anayesemekana kuwa Jose Mourinho.
Hakika
ubao wa matangazo wa dimba la Amsterdam mpaka dakika ya 90 ulikuwa
unasomeka 1-1 na watu wengi wakaamini timu hizo zinaenda kutumia sheria
nyingine ya mashindano.
Wakati
watu wakijiandaa kupata dakika nyingine, Ivanovic alichafua hali ya
hewa kwa Benfica na kuleta furaha kubwa sana kwa mashabiki wa Chelsea
waliosafiri kutoka London mpaka Uholanzi kuwashangilia vijana wao.
Haikuwa
kazi nyepesi kwa Chelsea kushinda mchezo wa jana usiku, lakini jinsi
walivyoonekana kujituma muda wote walionesha kuwa na umoja mkubwa sana
huku Kocha Benitez akiwahamasisha muda wake ili kubeba ndoo na kuondoka
kwa amani.
Wachezaji wa Chelsea wakibeba mwari wao baada ya kuwabamiza Benfica 2=1 katika uwanja wa Amsterdam
Chelsea wameongeza taji lingine kubwa baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barni ulaya mwaka jana
Frank Lampard akishika kombe lao
Peter Cech akiinua mzigo wao
Branislav Ivanovic akifunga bao lake na kusababisha ubao wa matangazo wa Amsterdam kusomeka 2-1
HUWEZI KUAMINI: Ivanovic akiwa amekalia mtambaa panya
VIJANA WAKE: John Terry akishangilia na watoto wake
MUDA WA KUFURAHI: Wachezaji wa Chelsea wakishangilia na mwari wao baada ya dakika 90 kumalizika
INAUMA SANA: Mashabiki wa Benfica wakionekana kuvunjika mioyo yao na kuumia zaidi ya kawaida baada ya kukosa ubingwa
Baada ya dakika 90, Chelsea wakishangilia ubingwa wao
FURAHA KUBWA: Lampard akiwashangilia kwa nguvu huku akiwatazama mashabiki wa Chelsea
VIKOSI VYA JANA
Kikosi
cha Benfica: Artur Moraes, Almeida, Luisao, Garay (Jardel 78),
Melgarejo (John 66), Perez, Matic, Rodrigo (Lima 65), Gaitan, Cardozo,
Salvio.
Subs Paulo Lopes, Aimar, Urreta, Gomes.
Booked: Garay, Luisao.
Goals: Cardozo (pen) 68.
Kikosi cha Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Lampard, Luiz, Ramires, Mata, Oscar, Torres.
Subs : Turnbull, Mikel, Moses, Ferreira, Marin, Benayoun, Ake.
Booked: Oscar.
MAGOLI: Torres 59, Ivanovic 90
MASHABIKI: 53,000.
MWAMUZI: Bjorn Kuipers (Holland).
Fernando Torres akifunga bao la kuongoza kwa upande wa Chelesea katika uwanja wa Amsterdam
Torres akishangilia bao lake jana
Chelsea walikuwa mbele kwa bao moja kabla ya Cardozo kusawazisha
Lampard akiwaangalia wachezaji wa Benfica wakishangilia baada ya kusawazisha bao na ubao kuonekana 1-1
Ivanovic ndiye aliyeamua jana katika dimba la Amsterdam na kuamua ubingwa kwenda kwao
Fernando Torres jana usiku amefunga bao la kwanza kwa Chelsea licha ya kuwa na ukame mkubwa wa kufunga mabao msimu huu
Bao
la Torres lilikuwa muhimu sana katika mchezo huo wa fainali ya kombe la
Ligi ya Uropa, hivyo ni historia kubwa sana kwake kuwepo darajani jijini
London
WACHEZAJI WA CHELSEA: wakimpongeza na kushangila sana baacda ya Ivanovic kuwapatia bao la ubingwa
AKIOKOA HATARI: Mlinda mlango wa Benfica Artur Moraes akiokoa shuti la Frank Lampard
MABEKI WAWILI SI MCHEZO: Nemanja Matic na Ezequiel Garay wakimzuia Torres
PRESHA KUBWA : Nyota wa Benfica Eduardo Salvio akifukuziwa na Torres
Bosi wa Chelsea Benitez akitoa maelekezo kwa wachezaji wake katika mchezo wa jana usiku
0 comments:
Post a Comment