Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Baada
ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 hapo jana dhidi ya JKT Ruvu ya
mkoani Pwani uwanja wa Chamazi, maafande wa Tanzania Prisons
“wajelajela” hawajasita kuelezea furaha yao na kusema kuwa sasa wapo
mikono salama na wanamshukuru Mungu pamoja na wakazi wote wa Mbeya
kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa hasa dakika hizi za lala salama.
Katibu mkuu wa Tanzania Prisons Sadick Jumbe ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa
ushindi wa jana umechangiwa na morali kubwa ya wachezaji wao ambao kwa
kiasi kikubwa waliahidi kupambana kufa na kupona mbele ya kamati ya
saidia Prisons ishinde inayoongozwa na mwenyekiti wake Kamanda wa Polisi
Mbeya, Diwani Athman Msuya huku naibu waziri wa elimu na mafunzo ya
Ufundi Philipo Mulugo akiwa miongoni mwao.
“Sasa
tuna uhakika wa kubakia ligi kuu msimu huu, shukurani kubwa kwa wana
Mbeya ambao kwa pamoja wameungana kutuunga mkono na sasa tunawakaribisha
wenzetu, klabu ya Mbeya city katika michuano ya ligi hii msimu ujao,
sasa mashabiki wa soka wataziona Simba, Yanga, Azam mara mbili kwa msimu
mmoja”. Alisema Jumbe.
Katibu
huyo wa wajelajela aliongeza kuwa sasa wamebakiza mchezo mmoja nyumbani
dhidi ya waliojeruhiwa jana baada ya kufungwa bao moja kwa bila na
Polisi Morogoro, nawazungumzia Kagera Sugar, mchezo ambao utakuwa mgumu
sana kutokana na Kagera Sugar kujiwekea malengo ya kutwaa nafasi ya pili
huku wakipoteza mechi ya jana na kubakia na pointi zao 40.
“Tunajua
Kagera ni wagumu sana, harakati za mapambano zinaendelea na haturudi
nyuma, mechi ya mwisho hakika hatulazi damu ndugu yangu, tuko na morali
kubwa na tunataka kuwaonesha mashabiki wetu kuwa tunatambua mchango wao
kwa asilimia zote”. Alisisitiza Jumbe.
Aidha
alisema mchezo wa kwanza kule kaitaba walifungwa mabo 2-0, lakini
kilichowaathiri ilikuwa ajali mbaya ya gari waliyoipata mzunguko wa
kwanza walipokuwa wanaenda mkoani Tanga kupambana na Mgambo, na baada
ya hapo walipumzika kidogo na kutibu wachezajim mwisho wa siku
walipoenda kaitaba wakafungwa.
“Kipindi
kile tulikwa wagonjwa, sasa tuko sawa, tutapambana kufa na kupona
kuhakikisha tunapata matokeo mazuri mechi hiyo ya nyumbani”. Alisema
Jumbe.
0 comments:
Post a Comment