Benchi
la Tanzania Prison linaloongozwa na kocha Jumanne Chale (wakwanza
kulia) katika moja ya michezo ya klabu hiyo msimu uliopita (Picha na
Maktaba)Mashabiki
wa Tanzania Prison katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka
Tanzania bara uwanja wwa Taifa (Picha na maktaba ya Glogalpublisher)
Na Baraka Mpenja
Wajelajela
Tanzania Prisons wameshaanza maandalizi ya kufanya usajili mapema ili
kuingia kambini mapema kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara msimu ujao ambapo wamesisitiza kuwa lazima waingie katika
kinyang`anyiro cha nafasi tatu za juu kama walivyokuwa wanafanya miaka
ya nyuma.
Katibu mkuu wa klabu hiyo Sadick Jumbe, ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa
viongozi wameshaona maeneo ambayo yamewasumbua sana katika harakati zao
za kukwepa mkasi wa kushuka daraja kuwa ni safu ya kiungo na
ushambuliaji.
“Sisi kama
viongozi tumekuwa tukifuatilia kwa karibu jinsi timu inavyocheza,
tumeona sehemu ya kiungo na ushambuliaji ina matatizo, tunafikiria
kuongeza nyota wapya ili kuhimili michuano ya ligi kuu msimu ujao ambao
tumehaha kweli kuutafuta”. Alisema Jumbe.
Jumbe
alisema kocha mkuu wa klabu hiyo Jumanne Chale bado anaandaa ripoti yake
ya ligi ambayo itajumuisha mapendekezo ya wapi kikosi kirekebishwe,
lakini viongozi kwa upande wao wameshaona wapi kuna matatizo wakati
wanasubiri mwalimu awasilishe ripotu kesho kutwa.
“Chale
ambaye tunamuamini sana anamalizia ripoti yake, itatumika akiwa ni
muongozo wetu kusajili, lakini tunajua sana wapi kuna matatizo, kwa
sababu yeye ni mtaalamu atatusaidia kupata wachezaji watakaotusaidia
zaidi”. Alisisitiza Jumbe.
Katibu
huyo alisema wamejifunza kitu, mwaka jana walisajili wachezaji ambao
hawakuwa na uzoefu, kwa sasa wanataka kutafuta wachezaji wenye uzoefu wa
kucheza ligi kuu ili wachanganyikane na wachezaji waliotoka nao ligi
daraja la kwanza.
“Unajua
wazoefu watasaidia kuongeza nguvu sana, ni muhimu sana kupata wachezaji
hao ingawa ni gharama kubwa, lakini halazi mtu damu, lazima tujipange
kwa gharama yoyote kupata angalau wachache”. Alisisitiza Jumbe.
Akizungumzia
safu ya ulinzi, Jumbe alisema walihangaika kidogo baada ya David
Mwantika kutimkia Azam fc, ila haiwapi presha kwani wameshapata mbadala
wake ingawa hakumtaja kwa sasa.
“Nadhani
watu wanaikumbuka sana Prisons iliyowahi kucheza kombe la shirikisho,
sasa inarejea msimu ujao, walitakiwa kutuombe dua mbaya tushuke daraja
ili kukwepa cheche zetu, tumefanikiwa kubaki, hakika tunaanza maandalizi
mapema mno na lazima tufanye makubwa msimu ujao”. Aliongeza Jumbe.
Pia
alisema kubakia ligi kuu msimu huu imekua faraja kubwa kwa mashabiki wa
Mbeya waliowapa sapoti kubwa sana hasa kipindi cha mwisho walichokuwa
wanachungulia kaburi.
Prisons msimu uliopita imemaliza katika nafasi ya tisa ya msimamo ikijikusanyia pointi 29 kibindoni.
Sasa Mbeya
itawakilishwa na timu mbili baada ya Mbeya City kufanikisha kupanda
daraja msimu uliopita na kupata nafasi ya kucheza ligi kuu pamoja na
Rhino Rangers ya Tabora, na wauza mitumba wa Ashanti United, huku timu
za Toto Africans, Africa Lyon na Polisi Morogoro zikiwa zimepisha njia
na kutimkia ligi daraja la kwanza.
0 comments:
Post a Comment